Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


DKT MWINYI AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZ

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Amesema  Miaka 60 ya Mapinduzi ni hatua kubwa katika mshikamano na umoja na kuwasisitiza Watanzania kuendelea kuenzi umoja huo ulioasisiwa na viongozi waliotangulia.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi zilizofanyika uwanja wa Amaan, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 12 Januari 2024.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi pamoja na shughuli mbalimbali alizopangiwa katika kufanikisha sherehe hizi.

Aidha , Rais Dkt.Mwinyi ametoa shukrani kwa wananchi wote,viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya siasa pamoja na  Viongozi wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao wameshiriki katika Maadhimisho hayo.

Vilevile katika kufanikisha sherehe hizo amemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Masoud Othman na kuipongeza Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho inayoongozwa na  Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdalla kwa kuyaratibu Maadhimisho hayo.

Halikadhalika amewapongeza Makamanda na Wapiganaji wa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Idara Maalum za SMZ  kwa kuonesha hamasa na gwaride la ukakamavu katika sherehe hizo.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ametoa shukrani kwa wageni kutoka nje ya Tanzania wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimaendeleo kwa kushiriki sherehe hizo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya SMZ na SMT waliohudhuria.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni, Rais wa Rwanda  Mhe.Paul Kagame,  Naibu Rais wa Kenya Mhe.Rigathi Gachagua, Waziri Mkuu wa Burundi Mhe.Gervais Ndirakobucha pamoja  na Viongozi Wakuu Wastaafu wa Serikali ya SMT na SMZ.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi