Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


CCM KIMBILIO LA WANANCHI, TUJADILI MAMBO YANAYOWAHUSU - WASIRA

alternative

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema Chama ni kimbilio la wananchi hivyo lazima kijadili na kubeba shida za watu.

Ameagiza vikao vya Chama vizungumzie mambo yanayowahusu wananchi kwa lengo la kusikia changamoto zao na kuwa sehemu ya kupatiwa ufumbuzi.

Wasira alieleza hayo mjini Bunda leo Januari 31, 2025 alipokutana na kuzungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Amesisitiza kuwa siyo sahihi vikao hivyo kujadili mambo yasiyo na maana wakati wananchi kjatika maeneo husika wanakabiliwa na changamoto ambazo endapo zitasikilizwa na kufikishwa mbele ya mamlaka husika zitapatiwa ufumbuzi.

“CCM ni lazima isikilize watu wanataka nini, sisi ni Chama cha watu na kwa kweli tunataka kiwe cha watu kwelikweli, vikao vyetu vya CCM vizungumze mambo ya watu, kama ni mambo ya wafanyabiashara wadogowadogo (machinga) tuzungumze kuhusu hilo, kama wana matatizo wakimbilie CCM kwa sababu wanajua huko ndiko kuna usalama.

Amesema kuwa, ni vema vikao vianze kusikiliza machungu yanayowagusa wananchi ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowqkqbili

“Unajua vikao hivi wakati mwingine mnajikuta mnajizungumza wenyewe badala ya kuzungumza wafanyabiasha wana matatizo gani, mama lishe wana matatizo gani, wakulima wana matatizo gani,” amesema.

== ==

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine