Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS SAMIA AMEFANYA KAZI YA VIWANGO VYA JUU, ZAWADI PEKEE NI KUMUOMBEA KWA MUNGU NA KUENDELEA KUMPA DHAMANA YA KUONGOZA TAIFA HILI - BALOZI DKT. NCHIMBI
"Watanzania tunaye kiongozi wa mfano sana anayefanya kazi yake kwa mapenzi makubwa ya watu wake anaowaongoza...wanasemaga nabii hakubaliki kwao lakini niwaambie ndugu zangu kuna nchi ambazo zingempata Rais Samia basi leo hii zingefika mbali sana, kuna baadhi ya nchi viongozi wao wakienda hata msibani nje ya nchi zao wanakwenda na ndege 7 na anakaa huko hata mwezi mzima akila raha tuu lakini sisi tunayae Rais ambaye kila anachokifanya ni kwa maslahi mapana ya watanzania na Taifa kwa ujumla"
"Rais Samia ametunukiwa shahada ya heshima ya udaktari (Honoris Causa) ya uchumi kutoka kwa Mkuu wa chuo cha Ankars kule nchini Uturuki, hii ni sifa kubwa sana kwa taifa letu kwakuwa hata wao wameona kazi kubwa anayoifanya katika Taifa analoliongoza katika masuala ya kuinuka kiuchumi na hili latupasa kujivunia kuwa na Rais Mchapakazi"
Aidha Balozi Dkt.Nchimbi amekumbusha kuwa siasa ya vyama vingi sio ugomvi, "Siasa ya vyama vingi sio ugomvi, tusiache kusalimiana na kupeana moyo sababu sisi sote ni watanzania, tushidane katika hoja na hapo ndipo tutatimiza dhamira ya Rais Samia ya kuwa na maridhiano na umoja , ndio maana Rais Samia alikubali kushiriki mikutano aliyoalikwa na CHADEMA na ACT Wazalendo"
"Anayetetea ugomvi hana dhamira njema kama kuna jambo basi tuzungumze, Baba wa Taifa aliwahi kusema kwa kutoa waraka kwa mabalozi wote, alisema " Jenga hoja, Usiropoke " mkiona watu wanajenga hoja basi kaeni nao, mkiona wanaropoka mara ugomvi mara kuandika ujinga kwenye mitandao watu hao wapuuzieni"
"Mtu anayechochea ugomvi katika jamii hana msaada kwa nchi yetu awe kutoka kwa chama chochote kile cha siasa"
"Tunataka kila kiongozi wa vyama vya siasa na serikali watambue kwamba wana wajibu wa kutambua na kulinda Amani ya nchi yetu"
"Tunaomba wananachi wote tuendelee kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuwa ameendelea kufanya kazi kubwa ya kuletea maendeleo kwa watanzania na taifa kwa ujumla"
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM
Akiuzungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Matarawe , Songea mjini Mkoani Ruvuma.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.