Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
BABATI VIJIJINI - MANYARA
Sekretarieti ya CCM Taifa inaendelea na ziara yake Mkoa wa Manyara ikiwa ni siku ya tatu (3) , Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ziara hiyo kuanza Mkoa wa Manyara ambapo leo tarehe 07 March 2023 Wamepokelewa katika Wilaya ya Babati vijijini na wanachama pamoja wananchi wa wilaya ya Babati vijijini kata ya Magala.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Daniel Chongolo ameambatana na Katibu wa NEC - Organaizesheni Ndg. Issa Gavu na Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Mjema.
Huu ni mwendelezo wa ziara ya Ukaguzi na Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika mkoa wa Manyara siku 6 na leo ni siku ya 3 anaingia Wilaya ya Babati Vijijini Mkoa wa Manyara.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.