WASIOTIMIZA WAJIBU WAO, WABINAFSI, SIKU ZAO ZINAHESABIKA - DKT NCHIMBI
Awataka wanaosuasua kukaza buti
Asema anaweza kula kiapo, Kamala alichukia rushwa
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewatahadharisha viongozi wote wanaotokana na CCM wasiotimiza wajibu wao kuwatumikia watu, kwa kadri ya matarajio ya Chama na wananchi, na badala yake wanatanguliza maslahi yao binafsi, siku zao zinahesabika, kwani CCM haiwezi kuwavumilia.
Dkt. Nchimbi amesema kuwa viongozi wote wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kuwa watumishi wa wananchi waliowachagua, wakiwatumikia kwa nguvu zao zote, wakiweka maslahi ya umma na Watanzania mbele wakati wote, kabla ya masuala yao binafsi.
Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akisisitiza namna bora ya kumuenzi Hayati Balozi (mst) Deodorus Buberwa Kamala, kupitia salaam za pole na rambirambi za CCM wakati wa shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu, iliyofanyika Februari 20, 2024, kijijini kwao Rwamashonga, Kata ya Bwanjai, Jimbo la Nkege, Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera.
Mbali ya kutoa salaam za Chama Cha Mapinduzi, Balozi Dkt. Nchimbi pia aliwasilisha salaam maalum za rambirambi kwa wafiwa na waombolezaji wote na kisha mkono wa pole kwa Familia ya Hayati Dkt. Kamala, kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo pia alieleza jinsi Rais Dkt. Samia alivyoguswa na msiba huo.
Balozi Dkt. Nchimbi ameongeza kusema kuwa mojawapo ya uwezo mkubwa wa kiuongozi aliokuwa nao Hayati Dkt. Kamala ni pamoja na saikolojia ya kutafuta suluhisho la changamoto za watu, tangu alipokuwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, huku akimwelezea jinsi alivyokuwa muadilifu, aliyechukia rushwa kwa vitendo, kiasi cha kuwa tayari kugharimu na kupoteza Ubunge wa Jimbo la Nkenge, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, kwa sababu ya hakuwa tayari kupokea fedha kuwasaliti wananchi wa jimbo hilo, aliokuwa anawatetea kwenye changamoto zao.
“Kamala hakuwa mla rushwa. Hili naweza kulisemea kwa kiapo. Hata alipopoteza ubunge, hakuwahi kulalamika. Kwa sababu alijua zile zilikuwa ni hela za udhalimu, hela za usaliti kwa wananchi wake. Watu wa namna hii lazima tuwaenzi vizuri kwa kutambua mchango wao mkubwa. Hongereni sana Misenyi kwa kuwa na Mwana wa Afrika wa namna hii. Mjisikie fahari sana. Nimefurahi hapa kusikia Mwenyekiti wa Halmashauri na Mbunge wa sasa (Jimbo la Nkenge) walivyoelezea mambo aliyofanya Dkt. Kamala na walivyo tayari kuyaendeleza na kufanya zaidi.
“Viongozi tunayo mengi ya kujifunza kwa watu kama Dkt. Kamala. Vijana mnayo mengi ya kujifunza kwa Dkt. Kamala. Hasa jinsi ya kutimiza wajibu kwa kuwatumikia wananchi. Kuweka maslahi ya nchi na kuwa na msimamo thabiti bila kigugumizi kwenye maslahi ya nchi. Na sisi Chama Cha Mapinduzi wajibu wetu tutawatetea na kuwalinda viongozi wanaotumikia wananchi na kutimiza wajibu wao.
“Wale viongozi wachache ambao bado wanasuasua katika kutumikia wananchi, tunawataka wakaze buti. Wale wachache wanaotanguliza maslahi yao binafsi mbele, ambao hawatimizi wajibu wao kuwatumikia wananchi, siku zao zinahesabika. Tunatakiwa kuwatumikia wananchi kwa nguvu zetu zote,” amesema Balozi Dkt. Nchimbi na kuongeza;
“Dkt. Kamala alikuwa na msimamo usioyumba kusimamia maslahi ya nchi. Kwenye vikao vya kimataifa, linapokuja suala la kutetea maslahi ya Tanzania, Kamala hakuwa na kigugumizi hata kidogo. Alikuwa na uwezo wa kusema bila kuangalia anaowakatalia wanatoka mataifa gani na watamfikiriaje, alikuwa hamwangalii mtu usoni anatokea wapi. Alikuwa na madhaifu yake kama binadamu lakini yanazidiwa na uwezo na nguvu .”
Hayati Dkt. Deodorus Buberwa Kamala, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge kwa nyakati mbili tofauti, kabla ya kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki na Waziri wa Afrika Mashariki na kisha Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Nchi ya Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya, mjini Brussels, alifariki Februari 12, 2024 na alizikwa Jumanne, Februari 20, 2024, kijijini kwake, Rwamashonga, Bwanjai.
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
25-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
25-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
25-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
25-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
25-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
25-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
25-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
25-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
25-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
25-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
25-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
25-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
25-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
25-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
25-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
25-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
25-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
25-05-2026