DR MWINYI AZIONYA TAASISI ZA SEREKALI ZINAZOKWEPA MATUMIZI YA MABADILIKO YA MIFUMO YA KISASA KWENYE UTENDAJI WAO
Alisema, kuna baadhi ya taasisi zinakiuka matumizi na miongozo ya mifumo iliyowekwa kisheria kwa utekelezaji na utendaji wa kazi zao, jambo alilolikataza mara moja kwani linakwamisha mipango na malengo ya Serikali. Dk. Mwinyi aliyasema hayo ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Kidijitali wa Serikali na Mfumo wa kitaifa wa Bajeti na Matumizi Serikalini (BAMAS). Aliwaagiza viongozi wa taasisi hizo wakiwemo Makatibu wakuu na wakuu wa taasisi
wanazozisimamia kuhakikisha wanapokea na kutumia mifumo ipasavyo kwa lengo la kujenga na kuimarisha miundombinu ya TEHAMA, sheria, miongozo, pamoja na taasisi zilizopewa majukumu ya kusimamia masuala hayo. “Nawaagiza viongozi wote wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali zote ikiwemo Mashirika na Taasisi za Kodi, Serikali Kuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kulisimamia agizo hili mara moja.” Aliagiza Rais Dk. Mwinyi.
Dk, Mwinyi alisema, Serikali itapunguza hujuma zinazofanywa na wachache kwa kutumia hati na nyaraka za kughushi na kuongeza mifumo imara, itatoa taarifa zilizotibitishwa kidijitali. Aliwaagiza Wakala wa Serikali Mtandao kupitia Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria,
Utumishi na Utawala Bora kushirikiana na Ofisi ya Rais - Fedha na Mipango, kutoa elimu kwa taasisi zote za Serikali na wananchi juu ya mkakati wa pamoja na matumizi ya Mifumo mipya ya serikali inayoendelea kuzinduliwa. Alieleza, mfumo huo pia utaimarisha sekta muhimu za kiuchumi, uwekezaji na ukusanyaji wa mapato nchini kwa kuzingatia mbinu na mikakati ya kuimarisha na kuendeleza sekta za utalii, uchumi wa buluu, kuharakisha utoaji wa huduma bora za Jamii, ikiwemo bima ya afya, kuimarisha biashara hasa kwa raia wageni hawatolazimika kufika Ofisi za Serikali kufanya miamala au usajili wa biashara na kampuni zao badala yake popote walipo watafanya hivyo kwa muda mfupi kupitia njia za kidijitali.
Pia Rais Dk. Mwinyi aliongeza mfumo itarahisisha shughuli za usajili wa wanafunzi kwenye Skuli na vyuo vikuu, usajili wa ndoa, vizazi na vifo. Mfumo wa BAMAS pia umeondoa changamoto za mifumo inayoendelea kutumika
sasa ya ukusanyaji mapato (Isidore) na Mfumo wa Matumizi (Epicor) na kueleza kwamba BAMAS umeleta uwazi kwenye Bajeti na Matumizi Serikalini kwa kuwezesha Mifumo yote ya Malipo na Matumizi ya Fedha za Serikali kusomana kwa haraka na kwa ufanisi. Alieleza matarajio yake kwa Mfumo wa BAMAS kwamba utaongeza nguvu ya udhibiti wa mali za Serikali, uwajibikaji kwa Watumishi na watendaji wa Umma na kuhakikisha fedha za Umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, ili kuwaletea wananchi maendeleo. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dk. Saada Mkuya Salum, alisema Mfumo wa BAMAS utaongeza ufanisi na utoaji wa huduma bora za Serikali pia utaunganisha pamoja sehemu ya mapato na matumizi
ya Serikali. Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora, aliiomba Serikali kuiongezea uwezo taasisi ya wa badala ya kuwa wakala kuwa
Mamlaka ili kuiongezea ufanisi na usimamiaji mzuri wa matumizi mtandao kwa taasisi zote za Serikali. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Serikali Mtandao Zanzibar, SaidiSeif Said alieleza kwa kipindi cha miaka miwili na nusu sasa wametengeneza na kusimamia mifumo 28 ukiwemo mfumo wa BAMAS na kueleza kwelekeo wa taasisi hiyo ni kuongeza kasi ya kutengeneza mifumo yenye nguvu zaidi ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa taasisi za Serikali.
Uzinduzi wa Mkakati wa Kidijitali wa Serikali na Mfumo wa Bajeti na Matumizi Serikalini (BAMAS) ulikwenda sambamba na kaulimbiu “Hatma yetu ipo viganjani mwetu”
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
24-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
24-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
24-06-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
24-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
24-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
24-06-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
24-06-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
24-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
24-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
24-06-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
24-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀!!
24-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐊𝐔𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐃𝐇𝐀𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐓𝐄𝐍𝐃𝐎
24-06-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐀𝐕𝐔𝐌𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐄𝐌𝐁𝐄, 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐆𝐀𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈
24-06-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀𝐀𝐀, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐀𝐍𝐙𝐈𝐀 𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈!
24-06-2026
𝐌𝐈𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟏𝟎% 𝐘𝐀𝐂𝐇𝐎𝐂𝐇𝐄𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐌𝐀𝐀𝐋𝐔𝐌
24-06-2026
𝐍𝐃𝐆 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐋𝐄𝐖𝐀 𝐑𝐔𝐕𝐔𝐌𝐀, 𝐀𝐇𝐈𝐌𝐈𝐙𝐀 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎 𝐍𝐃𝐈𝐎 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌
24-06-2026
𝐊𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐌𝐀𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
24-06-2026
𝐌𝐇𝐄. 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐀𝐍𝐀𝐖𝐀𝐏𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐒𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀, 𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐈𝐙𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐄𝐍𝐔 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐌𝐈𝐋𝐈𝐅𝐔: 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀
24-06-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐇𝐀𝐈𝐓𝐎𝐑𝐔𝐃𝐈 𝐍𝐘𝐔𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐋𝐀𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐋𝐈𝐌𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐎𝐑𝐎𝐒𝐇𝐎: 𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀
24-06-2026