Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewataka Viongozi, Watendaji na Wanachama kuepuka makundi yasiyofaa yanayoweza kuharibu umoja na mshikamano ndani ya Chama hicho

alternative

Kauli hiyo ameitoa wakati akiwahutubia Wanachama na Viongozi katika hafla ya ufungaji wa madarasa ya mafunzo ya Itikadi  iliyofanyika katika Ofisi ya Tawi la CCM Miwaleni Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kichama.

Alisema huu ni wakati wa wanachama na viongozi kushikamana zaidi katika kujiimarisha kisera,kisiasa na kiitikadi kwa nia ya kuendeleza utamaduni wa kuwa na wanachama wazalendo wenye kulinda maslahi ya Chama kwa vitendo.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa,alisema uimara wa CCM unatokana na uwepo wa wanachama waliojengewa uwezo kupitia madarasa mbalimbali ya itikadi na uzalendo na kwamba utamaduni huo unatakiwa kuendelezwa kwa kila jimbo ili kupata wanachama wapya walioiva kisiasa na kimaadili.

Alisema mkakati huo unatekelezwa kwa kufuata matakwa ya ibara ya 246 (e) inayoelekeza kufanyika kwa mafunzo ya Makada na Viongozi wa Chama kwa nia ya kuendeleza na kukuza elimu ya itikadi na uzalendo kwa wanachama wote.

“Chama chetu kimejengwa na mifumo imara  ya kisiasa na kiungozi toka enzi za TANU na ASP  wazee wetu waliona mbali na kutuwekea mifumo mizuri ya kuwapa mafunzo watu wanaohitaji kujiunga na CCM kabla ya kuwapatia uanachama na hiyo ndio tofauti ya CCM na Vyama vingine vya kisiasa”,alieza Dkt.Dimwa.

Dkt.Dimwa,alitoa wito kwa Maji na Wilaya za Chama Cha Mapinduzi zinazotoa mafunzo ya itikadi kuhakikisha wanafundisha na masomo ya ujasiriamali na uchumi wa buluu ili vijana waongeze ujuzi na ubunifu wa kutumia fursa zilizowazunguka kujiajiri wenyewe.

Aliwapongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa wanazofanya kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi.Mwaka Mrisho amesema Mkoa huo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi ibara ya tano ya Katiba ya CCM kwa kuhakikisha Chama kinashinda na kuchukua majimbo yote ya uchaguzi mwaka 2025.

Akizungumza Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman,alisema lengo la kuanzisha madarasa ya itikadi ni kuongeza wanachama wapya ambao ndio mtaji wa kisiasa wa kukipatia ushindi wa ngazi zote Chama Cha Mapinduzi.

Mhe.Haroun,aliwasihi wanachama na viongozi wa jimbo hilo kuweka kando tofauti zao zilizotokana na harakati za uchaguzi uliopita na badala yake washirikiane na kujipanga kikamilifu katika kutekeleza shughuli za kijamii na kisisa kwa ujumla.

Kupitia Dkt.Dimwa,aliwakabidhi kadi za uanachama wa CCM wanachama wapya 440 waliomaliza mafunzo ya Itikadi katika Madarasa saba ya Jimbo la Makunduchi.

 

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi