Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi jana jioni alijumuika na wananchi wa Mkoa wa kaskazini Unguja kwenye futari ya pamoja.
Futari hiyo maalum aliyowaandalia ukumbi wa VETA, kwenye Chuo cha Amali, Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni utaratibu uliojiwekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kila ifikapo Ramadhani kufutari pamoja na wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba na waumini wa dini ya kiislam katika kujenga umoja, ushirikiano, mshikamo na upendo na kuimarisha amani baina ya viongozi na wananchi.
Al hajj Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo, kuwashukuru wananchi hao kwa kuitikia wito wa kujumuika pamoja naye na kuuusifu uongozi wa Mkoa huo kugusa makundi yote ya jamii yenye uhitaji. Pia, Al hajj Dk. Mwinyi alisisistiza suala la kutunza amani, umoja, upendo, na mshikamano baina ya jamii ili kuyatunza maendeleo yaliopo nchini.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Hadid Rashid Hadid pia amemshukuru Rais Al hajj Dk. Mwinyi kwaniaba ya wananchi wa Mkoa huo kwa kuwafutarisha. Alisema zaisi ya wananchi 1300 walijumuika nayo kwenye futari hiyo wakijumuishwa na wananchi wa makundi yote wakiwemo wazee, wajane, wenye ulemavu, watoto, watoto yatima, wananchi wenye uhitaji, maimamu wa misikiti, walimu wa madrasa, wajasiriamali, wawakilishi wa asasi za kiraia na wawakilishi wa bodaboda.
Aidha, hafla hiyo ya futari ya pamoja pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.