𝐇𝐀𝐊𝐔𝐍𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐔𝐈𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐋𝐀𝐙𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐈𝐊𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐔𝐉𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐀 𝐍𝐀 𝐒𝐇𝐄𝐑𝐈𝐀
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema uchaguzi mkuu mwaka wa huu 2025 utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kwani mabadiliko yameshafanyika, hivyo hakuna atakayezuia uchaguzi.
CPA. Makalla ameeleza hayo leo Machi 4, 2025 wakati akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya Shina, Tawi, Kata na Wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.
“Uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa katiba kwa mujibu wa sheria, nimeona kwenye magroup yao wanaambiana wachangiane tone kwa tone tuchangiane tuende kwenye nguvu ya umma kuzuia uchaguzi, hela zitaliwa kwa sabaau uchaguzi utafanyika,” Amesema Makalla.
Akizungumza na Viongozi hao CPA. Makalla ameongeza kuwa kama watabaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi ni dhahiri baada ya uchaguzi mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakitokuwa na nguvu ya kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani nchini, kwani kwa kufanya hivyo kitaua ndoto za wengi wenye ndoto za kugombea udiwani, ubunge na viti maalumu kwani uongozi mpya utakuwa umefifisha ndoto zao.
“Kwahiyo Lissu namuhurumia anaingia katika historia ya kwenda kuiua Chadema ambacho ilikuwa inashiriki uchaguzi kilichokuwa kikipata wabunge na madiwani kupitia ndugu yangu anakwenda kuweka alama ya kwamba Chadema inakwenda kufutika kuwa sio chama cha upinzani kikubwa hapa Tanzania,” Amesema Makalla.
Aidha, CPA Makalla amesema kuwa ingekuwa ni busara na bora wangesema washiriki uchaguzi na baada ya hapo wakae na kukubaliana ili kufanya mabadiliko.
"Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliposikia hoja hizi za kufanyika mabadiliko ya uchaguzi kutoka kwa wadau mbalimbali aliunda kikosi kazi kwa ajili ya kukusanya maoni na kutoa ushauri juu ya sheria zilizopi na akamteua Prof. Mkandara kuwa mwenyekiti wa kikosi hicho ili kuweza kufanya mabadiliko." Alisema Makalla
Ameongeza kuwa, viliitwa vyama vyote kukutana na kutoa maoni na vyote vilishiriki isipokuwa CHADEMA kwani walisema walitaka kusikilizwa wakiwa peke yao na walimfata aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana walikabidhi taarifa kwa Mheshimiwa Rais na bila kusita uliandaliwa muswada wa sheria na kupelekwa bungeni.
Kamati ya bunge ilikaa na kukusanya maoni na ikapatikana sheria mbili ikiwemo sheria mpya ya Tume huru ya uchaguzi na kamati ya usaili itakayoongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Zanzibar na wajumbe fulani na katibu ya kamati ya tume ya mamlaka ambao watapeleka maoni ili rais aweze kuteuliwa.
Pia, CPA. Makalla alisema kupitia mabadiliko hayo Rais hawezi kubadilisha wala kuteua wajumbe wapga wa tume hadi kamati kuu ikae na kufanya maamuzi.
#CCMIImara
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee