Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amewataka Makatibu wa Wilaya,Mikoa,Wabunge na Wawakilishi nchini kufanya ziara za mara kwa mara za kusikiliza na kuratibu changamoto zinazowakabili wananchi.

alternative

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Wanachama wa CCM Jimbo la Pangawe Unguja,alisema Viongozi hao wana wajibu wa kusikiliza wananchi changamoto zao zitafutiwe ufumbuzi wa kudumu na mamlaka husika.

Dkt.Dimwa,alisema Wananchi wengi wanakabiliwa na changamoto zinazoweza kutafutiwa ufumbuzi kwa ngazi za Wilaya lakini zinashwa kufanyiwa kazi kutokana na uwepo wa urasimu kwa baadhi ya Watendaji.

"Chama Cha Mapinduzi ndio kimbilio la Wananchi kwani sisi tuna wajibu wa kuwasemea Wananchi ambao wengi wao sauti zao hazifiki sehemu husika lakini sisi tunafika hivyo tutekeleze wajibu wetu kikamilifu."alisema Dkt.Dimwa.

Alisema Chama Cha Mapinduzi ni daraja baina ya Serikali na Wananchi katika kutafsiri kwa vitendo dhana ya maendeleo endelevu katika nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu hiyo Dkt.Dimwa,alieza kuwa ufanisi wa kiutendaji wa Serikali na Chama  utaendelea kuimarika  endapo Viongozi na watendaji watakuwa karibu na Wananchi.

Pamoja na hayo alisisitiza kufanyika kwa Vikao vya ngazi za Matawi na Mashina ili kujadili masuala ya msingi yanayowahusu Wanachama wa CCM kwa lengo la kuziwasilisha ngazi husika kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi.

Kupitia Mkutano huo,alitaka kuimarishwa kwa mikakati ya kuongeza Wanachama wapya ambao ni mtaji wa kisiasa wa CCM hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2025. 

Pamoja na hayo alisema msimamo wa CCM nikutekeleza kwa vitendo ibara ya 5 ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la Disemba 2022 inayoelekeza Chama kushinda Uchaguzi Mkuu na Serikali za Mitaa kwa Tanzania bara na Zanzibar.

alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi