RAIS DK. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWAAHIDI WANZANZIBARI KUWAPUNGUZIA UMASIKINI KABLA YA MWAKA 2025 KWA KUWAONGEZEA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO.
Amesema, amekusudia kuikamilisha kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025 kwa miaka miwili iliyobakia ya uongozi wake na kuikamilisha miradi mkikubwa ya kimkakati ya Bandari Jumuishi ya Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, barabara za kutulia na kurukia ndege pamoja na jengo kubwa la abiria katika uwanja wa ndege wa Pemba vinavyotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekeni milioni 400.
Dk. Mwinyi ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM- Zanzibar aliyasema hayo, viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, alipozungumza na Wazanzibari kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wake, tokea alipoingia madarakani kuiongoza awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mwezi Novemba mwaka 2020.
Pia, Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya Zanzibar na kuongeza kuwa hatua ya maendeleo iliyofikiwa ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba kuna mkono wa Rais Dk.Samia. Akizungumzia suala la amani, umoja na mshikamano, Rais Dk. Mwinyi alisema maendeleo makubwa yaliyofikiwa Zanzibar ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, yametona na juhudi kubwa ya wananchi wa Zanzibar, kuendelea kuidumisha amani iliopo, umoja na mshikamano wao, umetoa fusra nzuri ya kutendeka mafanikio yote hayo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliahidi kuongeza tena kasi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili iliyobakia. Pia aliwapongeza Umoja wa Wanawake Tanzania, (UWT) kwa kazi kubwa wanayoifanya nchi nzima, kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na miradi ya Maendeleo Tanzania bara na visiwani.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyeketi wa UWT Taifa, Merry Chattanda alipongeza juhudi kubwa ya mafanikio iliyofikiwa na awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye sekta zote za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabra, Skuli, hospitali 10 za wilaya na moja ya mkoa iliyokamilishwa kwa miundombinu na vifaa vya kisasa, ongezeko la ajira kwa vijana kupitia sekta za ujenzi wa miundombinu, utalii, ujasiriamali, biashara na kilimo cha umwagiliji wa mpunga, hali aliyoielezea matarajio ya Zanzibar kujiwekea akiba ya chakula.
Pia, Chattanda alimpongeza Rais. Dk. Mwinyi kwa kufanikiwa kuwakomboa wanawake wa Zanzibar dhidi ya changamoto cha maji safi na salama kwa kuwajengea visima vikubwa vya maji, Unguja na Pemba pamoja na kuwasambazia mabomba, kuwawekea usafiri wa haraka baharini kisiwani Pemba.
Aidha, Chattanda alisifu mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation kupitia Mwenyekiti wake wa Bodi, Mama Mariam Mwinyi, Mke wa Rais wa Zanzibar kwa kuwezesha kinamama wengi wakulima wa mwani na kuwajengea kiwanda kikubwa cha kusarifu mwani, eneo la Chamanangwe, Pemba. Mapema, akiwasilisha salamu za Chama cha Mapinduzi viwanjani hapo, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Abdul Rahman Kinana aliwasihi Wazanzibari kuendelea kuidumisha amani na mshikano uliopo baina yao na kuendelea kushirikiana na viongozi wao wa Serikali kuijenga Zanzibar.
Sherehe za maadhimisho ya miaka mitatu ya mafanikio ya awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilliandaliwa na kufanikishwa na Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wanawake, Tanzania (UWT)
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025