Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Alhaj Dkt.Mohamed Said Dimwa,amewasihi waumini wa dini mbalimbali nchini kufuata falsafa na maoni ya aliyekuwa Rais wa awamu ya pili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na Rais wa awamu ya tatu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Ali Hassan Mwinyi.
Wito huo ameutoa wakati akizungumza katika hitma ya kumuombea marehemu Mzee Mwinyi iliyofanyika katika msikiti wa Donge Pangamaua Jimbo la Donge,amesema kiongozi huyo enzi za uhai wake amekuwa ni mfano wa kuigwa katika maisha yake ya uongozi na baada ya kustaafu kwa kuishi katika misingi ya maadili,uadilifu na ucha Mungu.
Alhaj Dkt.Dimwa,alisema Mzee Mwinyi atabaki katika kumbukumbu na historia ya kipekee katika kulinda,kutetea na kuendeleza misingi ya uongozi bora wenye kufuata matakwa ya kidemokrasia kwa wananchi na alipinga tabia za ubaguzi wa kidini,kikabila na kisiasa.
“Zawadi kubwa ya kumpatia Mzee wetu huko aliko ni kumuombea dua kwa wingi ili Mwenyezi Mungu amjaalie mema,nasi tuendeleze pale alipotuachia kwa kuhakikisha tunaishi katika misingi ya maadili mema ya ushirikiano,upendo na kudumisha amani na utulivu”, alisema Dkt.Dimwa.
Aliwasihi waumini hao na wananchi kwa ujumla kuwarithisha watoto wao misingi ya maadili mema katika malezi yao ya kila siku ili kupata viongozi bora wa sasa na baadae.
Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa,alieleza kuwa kila mwananchi ana jambo la kujifunza juu ya maisha ya Mzee Mwinyi harakati za kiungozi,kidini,kitamaduni na kisiasa.
Kupitia hitma hiyo Dkt.Dimwa,alitoa salamu za Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kuwa anawashukru wananchi wa Jimbo la Donge na majimbo jirani wanaofanya hitma na dua mbalimbali za kumuombea kiongozi huyo Mzee Ali Mwinyi aliyeongoza Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Katika hitma hiyo iliyoandaliwa na Jimbo la Donge iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwakilishi wa Jimbo hilo Dkt.Khalid Salum Mohamed,Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid pamoja na Madiwani na wananchi wa jimbo hilo.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.