Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, iliyoko jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 15-7-2024, na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kampuni ya Infinity Group Bw. Samuel Saba na ( kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar. Mhandisi.Ali Said Bakari, akitowa maelezo ya mnara ulioko katika bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. unaoonesha masafa ya maeneo mbali mbali ya Unguja yanayoazia katika enao hilo, wakati wa ufunguzi wa bustani hiyo uliyofanyika leo 15-7-2024.(Picha na Ikulu)
NO.2324///RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kuifungua Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 15-7-2024, iliyoko jirani na Hospitali ya Mzani Mmoja.(Picha na Ikulu)
NO.2336-2346-2395///BAADHI ya Wageni waalikwa katika ufunguzi wa Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi. (hayupo pichani) akizungumza na kuifungua bustani hiyo ufunguzi huo uliofanyika leo 15-7-2024.(Picha na Ikulu)
NO.2371////RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua leo 15-7-2024, akiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.(Picha na Ikulu)
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.