Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


RAIS SAMIA AAHIDI KUENZI MAONO YA HAYATI  MZEE ALI HASSAN MWINYI

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt  Samia Suluhu Hassan  ameongoza Maelfu ya waombelezaji akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassani Mwinyi  aliyefariki tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.

Akihutubia wananchi Rais Samia amesema kuwa ataendelea kuyaenzi na kuyaishi  maono ya Mzee Ali Hassan  Mwinyi kwa kusimamia  ustawi wa wananchi na kushamirisha sekta binafsi sambamba na kutenda haki kwa raia.

Hafla hiyo ya kuaga mwili imeambatana na Dua iliyofanyika katika viwanja  vya Amaan Mjini Magharibi Unguja.

Viongozi wengine walioshiriki katika Ibada hiyo ya Mazishi ni pamoja na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Kassim  Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla na Rais Mstaafu wa Awamu ya Saba Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein na Viongozi wengine wa Kimataifa.
 

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi