Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MAKALLA: RAIS SAMIA AMEMUELEKEZA  WAZIRI MKUU KUFIKA SOMANGA

alternative


- Awatoa hofu wananchi mikoa ya kusini mawasiliano yataendelea kuimarishwa
- Rais Samia ametoa fedha sh Bilioni 100 kujenga madaraja

MTWARA: RAIS Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufika katika daraja la Somanga Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kesho ili kuhakikisha mawasiliano yanarejea katika barabara ya kutoka Dar es salaam kuelekea mikoa ya Kusini.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla  ameeleza hayo leo Aprili 15,2025 akiwasalimu wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Tandahimba, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 10 mkoa wa Lindi na Mtwara.

Makalla amewatoa hofu wananchi wanategemea barabara ya kusini na kueleza kuwa serikali chini ya uongozi wa Rais Samia inatambua tatizo hilo lililosababishwa na mvua zinazoendelea na jitihada zinafanyika kuhakikisha mawasiliano yanarejea.

“Niwatoe wasiwasi Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi na Rais, Dk Samia Suluhu Hassan asubuhi ya leo amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kesho anatia timu pale ili kuhakikisha mawasiliano ya mikoa ya kusini yanarejea,” amesema Makalla.

Ameongeza kuwa CCM inadhamana kwa wananchi kwa sababu inashughulika na changamoto zao, hivyo jitihada kubwa zinafanyika kuhakikisha wananchi wanaotumia barabara hiyo wanaendelea kupata huduma za usafiri wakati ujenzi wa madaraja ya kudumu ukiendelea.

Aidha, Makalla ameeleza kuwa alipoanza Ziara yake katika mikoa hiyo alipita katika eneo la Somanga na kuikuta Wizara ya Ujenzi pamoja na wakandarasi wakiwa kazini wakiendelea na kazi ya kurudisha mawasiliano na kuendelea kusimamisha nguzo kwa ajili ya kukamilisha daraja.

Ameongeza kuwa mawasiliano yalirejea na barabara hiyo ikawa inapitika lakini bahati mbaya kutokana na mvua zilizonyesha juzi katika maeneo mengine zimesababisha daraja hili kukatika na mawasiliano katika barabara hiyo kupotea kwa masaa kadhaa lakini asubuhi yameanza kurejea na magari yalianza kupita.

alternative alternative
Habari Nyingine