Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


MIRADI YA MAENDELEO NI MATOKEO YA USIMAMIZI MZURI WA RASILIMALI

alternative

 

•Amtaja Dr Samia Suluhu ni mzalendo na anaipenda Tanzania

GAIRO: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chma Cha Mapinduzi (CCM)makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa Rais muadilifu kwani amekuwa na uwezo mkubwa wa kupeleka fedha za maendeleo katika maeneo mbalimbali.

Pia amesema fedha na rasilimali zote zinazokusanywa zimapelekwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kueleza miradi mikubwa ya maji, madaraja ambayo ilishindikana kwa miaka mingi, barabara, hospitali na mengineyo.

Makalla amesema hayo leo Mei 16, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Motogogoro wakati akihitimisha ziara yake iliyoanza mapema mwezi huu mkoani humo.

“Kwahiyo katika Tanzania kiongozi namba moja anayewapenda Wanzania na aliyeapa kuilinda Tanzania na rasilimali zake zote ni Rais Samia Suluhu Hassan na ndo maana anaingia katika rekodi ya marais waliopeleka fedha za maendeleo kuliko awamu yoyote,” amesema Makalla.

Makalla ameongeza anayesema Tanzania haina maendeleo anahitaji kupimwa akilibkwani maendeleo yaliyofanyika haya hitaji tochi kuyatazama na frdha kwa ajili ya kufanya maendeleo hayo zinatolewa na Rais Samia ambaye ameonesha kuwa rais wa kuahidi na kutenda.

alternative alternative
Habari Nyingine