Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KATIKA SIASA SHUKRANI ZINATAFUTWA, NI LAZIMA USEME ULIYOAHIDI NA ULIYOTEKELEZA - KATIBU MKUU DKT. NCHIMBI
> Atoa pongezi kwa wana katavi kwa mapokezi na hamshahamsha nzuri yenye kujaa neema.
> Awashukuru kwa kufuatilia kwa karibu siasa za kitaifa haswa kwa kauli yao ya taa zote kuzimwa na kubaki ya CCM
> Asema Utaratibu wa utawala bora katika kutekeleza sera za CCM ni kusimamia utawala wa sheria.
"Taarifa tuliyopokea ya utekelezaji wa Ilani Mkoani Katavi inatia moyo sana kutokana na kupunguza maswali mengi kwa wananchi ila kinachotuponza siku zote ni kutosema kazi kubwa tunayofanya na badala yake kinachotuponza ni kufanya kama ile msemo usemao tenda wema uende zako."
"Niwaambie sasa katika siasa shukrani zinatafutwa ni lazima ueleze uliyoahidi na uliyotekeleza usiposema watakuja wenzako watasema walifanya wao"
"Wapo wanasiasa wanangoja mfanye kazi baadae wanakuja wao wanasema wao ndio wamefanya"
"Sote tunajua zipo serikali duniani hazitimizi miradi yao lakini sisi viongozi wetu wanatumia mapato ya umma kuleta maendeleo, tusione haya na tutoke tuseme kazi kubwa imefanywa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mqenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na hii ndio changamoto ya viongozi wetu kutosema"
"Maeneo machache yenye mapengo tutaziba, nafasi yetu ya kuismamia serikali tutaifanya kwa usiamamizi madhubuti na wenye staha."
"Utaratibu wa utawala bora katika kutekeleza sera za CCM ni kusimamia utawala wa sheria, wajibu wetu ni kuzihamasisha na kuziwesha mahakama zetu ziweze kutenda haki"
"Nchi inayotaka kusimamia sheria lazima kujenga utaratibu wa kuzingatia utawala wa sheria"
Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM
Akizungumza wakati akitoa salamu kwa Viongozi, wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau mbalimbali waliojitikeza kwa wingi kuwapokea katika ofisi za CCM mkoa wa Katavi.
🗓️ 13 Aprili, 2024
📍Mkoa wa Katavi
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.