Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
KINANA: SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA ITACHUKUA HATUA KUKABILI ATHARI ZA MVUA.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ujumla inafuatilia kwa karibu athari zinazotokana na mvua kubwa ikiwemo kusababisha uharibifu wa miundombinu.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupeleka fedha za ukarabati wa miundombinu na misaada mbalimbali kuwasaidia walioathirika.
Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini ambao walieleza uharibifu wa baadhi ya miundombinu ya barabara katika wilaya hiyo na Mkoa wa Mara kwa ujumla kutokana na mvua zinazoendelea kunyeesha.
"Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu huo wa miundombinu ili kutenga fedha za kukarabati maeneo yote ambayo yameathirika.Uharibifu wa miundombinu umefanyika katika nchi mbalimbali duniani hata zile zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo na sio Tanzania peke yake.
"Kwa mara ya kwanza tumeona duniani nchi nyingi zimepatwa na mafuriko, hata zile ambazo katika historia hatukuwahi kuona mvua, hivyo sio sisi peke yetu, haya yote yametokana na mabadiliko ya tabianchi, mahitaji ya kufanya marekebisho ni makubwa na yataendelea.
"Niwaambie Rais Samia anapata taarifa kuhusu haya yanayotokea katika mikoa mingi, sehemu ambapo miundombinu imeharibika sana hadi kukosekana kwa mawasiliano hatua za dhati zimechukuliwa," amesema.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.