Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
BALOZI NCHIMBI ASIMAMISHWA NDANDA, AMPIGIA SIMU WAZIRI TAMISEMI, NAE APOKEA MAELEKEZO UJENZI WA KITUO CHA AFYA
▶ Asisitiza wananchi kuendelea kulinda amani, utulivu na mshikamano nchini
▶ Atoa wito kwa Serikali kuhakikisha wakulima wanakuwa salama na wafugaji pia kwani wanategemeana .
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, 28 Julai ,2024 akiwa njiani kuelekea Mtwara Mjini baada ya kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa Masasi amesimamishwa na wananchi katika eneo la Kata ya Nganganga Jimbo la Ndanda wakitaka awasalimie na kuzungumza nao.
Akiwa hapo Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameendelea kuwasisitiza Watanzania kuhusu umuhimu wa umoja wa kitaifa kwa kutunza tunu ya amani iliyopo nchini, pamoja na kumpigia simu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akitaka kujua utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya, ambapo Waziri alipokea maelekezo na kuahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi ujao baada tu ya mwaka wa fedha kuanza.
Katibu Mkuu wa CCM na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anaendelea na ziara ya mikoa miwili inayolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020/2025, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.