CHONGOLO AANZA NA UMEME, AKITUA KATAVI ZIARA YA SIKU 5
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Godfrey Chongolo amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa Chama hicho kitasimamia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maeneo ya mkoa huo, utakaopatikana kwa kuunganishwa na gridi ya taifa.
Akizungumza na wanachama, viongozi wa CCM na wananchi wa Mpanda Mjini, Jumatatu Oktoba 2, 2023 katika ofisi za chama hicho Mkoa wa Katavi, mara baada ya kuwasili mkoani humo, kuanza ziara ya kikazi, Ndugu Chongolo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia changamoto ya kukosekana kwa umeme wa kutosha katika mkoa huo kutokana na kutounganishwa na gridi ya taifa.
“Suala la kuunganisha laini ya umeme wa gridi ya taifa kutoka Tabora kuja Mpanda, ujenzi wa vituo va kupoza umeme tayari vimeshamilika. Lakini umeme wa kupokelewa ili upozwe ndiyo haupo. Subira imekuwa ndefu.Nimeambiwa viongozi kadhaa wamekuja kuelezea hilo na kutoa maelekezo kadhaa na maagizo ili Mpanda na Nkasi wapate umeme wa uhakika.
“Sisi tuliahidi mikoa hii yote ambayo haijaunganishwa na gridi ya taifa tuhakikishe inaunganishwa katika kipindi cha miaka hii mitano ya utekelezaji wa Ilani.
“Kigoma wameshaunganisha kwa sehemu kubwa ya mkoa, Rukwa tayari bado Mkoa wa Katavi. Niwaahidi ninatamani kuchaguliwa kwa kishindo katika mkoa huu Chama Cha Mapinduzi , ni matamanio yangu hayo ni kutokuwa na ahadi hewa itakayotusumbua au kutupatia maswali huko mbele.” amesema Chongolo.
Amewaambia wananchi atazungumza na Waziri wa Nishati ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo.“Nitawaita wanaohusika na hili jambo , huu mradi unafanywa na TANESCO.
“Hivyo niachieni nitaenda kukaa na Waziri anayehusika na TANESCO bahati nzuri amepewa mamlaka makubwa kwa hiyo hana sababu ya kujitetea.Nitakwenda kumwambia aje kuangali uhalisia wa utekelezaji wa huu mradi.
“Pili ahakikishe anaweka nguvu zake hapo ili wananchi wa Mkoa wa katavi sasa na wao wapate umeme wa gridi wa taifa na sio vinginevyo.”
Akieleza zaidi amesema ameambiwa na Mkuu wa Mkoa kwamba watu wengi wanataka kuwekeza katika viwanda vikiwemo vya kuchakata alizeti na tumbaku lakini changamoto ni umeme wa uhakika.
“Sisi lazima tuwe mbele ya wananchi , sio wananchi watangulie hatutawandea haki.Ni lazima tuhakikishe tunalifanyia kazi.Kazi yangu ni rahisi kwenda kusimamia kuhakikisha tuliyokubaliana tunatekeleza.
“Naenda kusuma mradi huu, hatuwezi kuwa na barabara nzuri kutoka Tabora kuja hapa halafu umeme tu wa kuunganisha nguzo ukatushinda.”
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
19-03-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
19-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
19-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
19-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
19-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
19-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
19-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
19-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
19-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
19-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
19-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
19-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
19-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
19-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
19-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
19-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
19-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
19-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
19-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
19-03-2026