Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


TUTUNZE AMANI-MJEMA

alternative

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Mjema, amewasihi Watanzania kutunza amani ya nchi.

Ameyasema hayo leo tarehe 17 Oktoba, 2023 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kata Sudi, Lindi Vijijini.

"Amani ya nchi tuitunze ndugu zangu, kuna nchi nyingine mtoto anazaliwa hadi anazeeka ni milio ya mitutu tu, maendeleo yanapatikana katika amani," amesema Ndg. Mjema.

Ndg. Mjema ambaye alikuwa mkoani Lindi kuendesha mafunzo ya falsafa, itikadi na sera za CCM kwa viongozi na watendaji wa CCM, amesema demokrasia itumike kuimarisha amani.

Amesema fursa ya demokrasia nchini inatokana na uongozi makini wa CCM, na kimekuwa kikiitekeleza ndani ya chama kwa vitendo.

Amewataka  wananchi kuchuja maneno wanayoambiwa au kuyasikia kutoka katika majukwaa ya siasa.

Amesema wako wanasiasa wanasema uongo na kuwataka wananchi waachane nao.
 
Amesema wananchi NI mashahidi kwamba chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nchi inasonga mbele katika maendeleo.

Amesema katika kipindi kifupi, tangu amekuwa Rais, maendeleo makubwa katika kila sekta yamepatikana.

"Vituo vya afya, shule, maji, barabara, umeme, taja chochote, hakuna kilichosimama, mabilioni ya fedha yanashuka hadi vitongojini," amesema. 

Ndg. Mjema amesema katika uchaguzi mkuu wa 2020, CCM iliahidi maendeleo kwa Watanzania na sasa inatekeleza.

"Usidanganywe na mtu, CCM imeahidi imetekeleza na kazi inaendelea," amesema na kuongeza kwamba "mtu ukimpa nafasi akakudanganya, maana yake anakudharau."

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi