Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya

alternative

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii, vifichue maovu na kutowajibika kunakofanywa na Watumishi na Watendaji wa Serikali,vinatoa mrejesho wa hisia na mtazamo wa wananchi kwa Serikali yao, na kwa ujumla, vinafanya kazi ya kuelimisha na kukuza demokrasia.

Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa masuala haya ndiyo yanayoifanya Serikali kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na vyombo vya habari.

Vyombo vya habari sio mshindani wa Serikali bali ni mdau na mshiriki muhimu katika yanayotendwa na

Serikali hivyo, Serikali itaendelea kuweka mifumo mizuri ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi, katika kuimarisha uhuru na mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari.

alternative alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi