Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuweka mazingira mazuri kwa kuziimarisha Taasisi za Ujenzi ili kuhakikisha wataalamu wazawa wanakuza taaluma zao na kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa Miradi inayojengwa na Watanzania
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa mafunzo ya kuwaendeleza wataalamu wa Usanifu, Uhandisi na Wakadiriaji Majengo Tanzania hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Maonesho Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Amesema kuwa Serikali zote mbili zimetoa kipaombele kwa wataalamu wa Ujenzi na Makampuni ya ndani ya nchi kupitia Wizara na Taasisi ambazo zimefanya jitihada maalum za kuweka Sera, Sheria na kanuni zenye vigezo rafiki ili kurahisisha maombi ya kazi za ujenzi hapa nchini.
Mhe. Hemed amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuitumia vyema nafasi waliyoipata ili kuweza kupata uwelewa mkubwa na mbinu mbali mbali za ujenzi ikiwemo utumiaji wa njia mbadala ya vyuma hasa Zanzibar ambapo kumekuwa na uhaba mkubwa wa matumizi mali zisizorejesheka kama vile mchanga na nyenginezo.
Aidha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema matumaini makubwa ya Serikali kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuonesha mbinu za kuhifadhi, kuitunza na kuiendeleza miji ya urithi ambayo inachangia kuongeza pato la Taifa kupitia watalii wanaokuja nchini
Sambamba na hayo ametoa wito kwa Makampuni na wataalamu wa Ujenzi kuendelea kuwa waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuzingatia ubora unaohitajika na muda wa mradi uliopangwa ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa na kudumu kwa muda mrefu kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.
Akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiano na Uchukuzi Katibu Mkuu Wizara hio Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema kufanyika kwa mafunzo haya kunatokana na mashirikiano yaliyopo kwa Pande mbili za Muungano kwa lengo la kuhakikisha tunakuwa na wataalamu wabobevu hasa katika masuala ya kutunza na kuboresha Miji ya Urithi wa dunia.
Dkt Mngereza amesema ushirikiano uliopo katika Sekta za Ujenzi kwa Tanzania Bara na Zanzibar Umesaidia kuimarika kwa Miundombinu ya Barabara na kupelekea kuongezeka kwa Kipato Kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla pamoja na kuimarika kwa huduma za kijamii.
Kwa upande wao Wenyeviti wa Bodi ya Usajili wasanifu, wahandisi na wakadiriaji majengo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wamezishauri Serikali kutumia wataalamu wazalendo katika shuhuli za ujenzi ili majengo na Miji ya Urithi iweze kuwa bora zaidi.
Wamesema wakati umefikwa kwa Serikali kuangalia sheria na miongozo katika masuala ya ujenzi ili kupunguza changamoto ya kujengwa kwa majengo yasiokidhi viwango na ubora na kuendelea kulitia hasara Taifa siku hadi siku
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025