Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuchukua hatua mbali mbali pamoja na kutekeleza mkakati wa usalama barabarani mwaka 2024-2030 ili kuhakikisha inaondosha uwepo wa ajali za barabarani.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya kwanza ya wiki ya usalama barabarani na uzinduzi wa mkakati wa usalama barabarani Zanzibar yaliyofanyika katika Ukumbi wa viwanja vya Maonesho Nyamanzi Zanzibar.
Amesema kuwa kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua na kuondoka kabisa kwa kuchukua tahadhari mbali mbali ili kuepuka madhara yatokanayo na ajali hizo ikiwemo vifo na ulemavu wa kudumu.
Makamu wa Pili wa Rais amesema Tafiti mbali mbali zinaonesha kuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani zinatokana na makosa ya kibinaadamu yanayo sababishwa na madereva kutokufuata sheria za usalama barabarani, kutembea kwa mwendo kasi, Ulevi, kutumia simu wakati wanaendesha magari, ubovu wa magari, uchakavu wa miundombinu ama hali ya hewa.
Amesema jamii inapaswa kuzitumia Tafiti hizo ili kusaidia kuonesha chanzo cha tatizo na namna ya kutatua tatizo hilo ikiwemo la ajali za barabarani Unazoendelea kugharimu maisha ya watu na mali zao.
Aidha , Mhe Hemed amesema kuwa takwimu zinaonesha kuanzia mwaka 2019 hadi 2023 jumla ya ajali za barabarani 1,181zimeripotiwa kwa vyombo husika zilizosababisha vifo 799 na majeruhi 1,461 ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba 2024 ajali 193 zimeripotiwa na kusababisha vifo 264 na majeruhi 216.
Sambamba na hayo, ameiagiza Kamati ya Kitaifa ya Uaalama barabarani kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kisheria ikiwemo kutoa elimu ya usalama barabarani kwa jamii na kulitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha sheria za usalama zinafuatwa kikamilifu na kuwachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na sheria hizo.
Hata hivyo Mhe. Hemed amewataka maderva wote wa vyombo vya usafiri barabarani kufuata sheria za usalama barabarani na kuhakisha uimara wa vyombo vyao kabla ya kuingia Barabarani pamoja na wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kwa vyombo vinavyosimamia usalama barabarani kwa kutoa taarifa wanapogundua dereva ama madereva wanakwenda kinyume na sheria hizo.
Nae Waizi wa Ujenz, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Dkt Khalid Salum Muhammed amesema ajali za barabarani ni jangla Taifa linaloendelea kupoteza maisha ya wanachi, kupata ulemavu wa kudumu, pamoja na upotevu wa mali zao kupanda kwa gharama za matibabu jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa kwa wanaopatwa na majanga ya ajali za barabarani.
Dkt. Khalid amesema mashirikiano ya pamoja yanahitajika katika kuhakikisha kila mmoja anafuata sheria za usalama barabarani, kutolewa elimu ya matumiza salama ya barabara ili kumaliza kabisa jangla ajali za barabarani.
Amefahamisha kuwa katika harakati za kupambana na kupunguza ajali za barabarani lazima kuwepo na mazingatio ya mipango miji kwani wimbi la ujenzi holela hasa pembezoni mwa barabara limekuwa likiongezeka jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa ajali za barabarani
Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Rais Dkt Hussein Mwinyi za kuleta maendeleo hasa katika Sekta ya Miundombinu ya Barabara na kuakisi dhamira yake ya kuimarisha Usalama Barabarani na kutokomeza kabisa ajali zinazosababishwa na madereva, wamiliki na wananchi kutokufuata sheria za Usalama barabarani.
CP Hamad amesema kikosi cha Usalama Barabarani kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo watumiaji wa barabara kutokuwa na elimu ya usalama barabarani hivyo ameshauri kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya barabara na kufuata sheria za usalama barabarani.
CP Hamad amesema madereva wengi wamekuwa hawafuati sheria pindi wanapokuwa barabarani na kusababisha ajali zinazogarimu maisha ya watu na mali zao hivyo amaeshauri kutumika kwa Teknolojia ya kisasa ili kudhibiti mwendo kasi na kuwatambua wavunjifu wa sheria za usalama barabarani na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine ambao hufanya makosa kama hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wadhamini wengine wa Hafla hio Bibi AWENA RAJAB MOH’D kutoka Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA) amesema ongzeko la ajali limekuwa janaga la Taifa ambapo hatua za dharura zilipaswa kuchukuliwa ili kudhibiti janga hilo ambalo linaendelea kuteketeza maisha ya wananchi wengi nchini.
Amesema ZICTIA inaamini kuwa elimu iliyotolewa katika wiki ya usalama barabarani imewafikia walengwa na itatotoa matokeo chanya hasa katika kufuata sheria za usalama barabarani bila shuruti na kuachana na yale yote yanayopelekea uvunjifu wa sheria na kusababisha vifo, ulemavu wa kudumu na kupotea kwa mali za wananchi.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
26-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
26-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
26-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
26-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
26-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
26-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
26-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
26-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
26-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
26-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
26-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
26-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
26-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
26-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
26-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
26-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
26-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
26-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
26-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
26-10-2025