Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salama za pole kutoka kwa kampuni ya WASAFI inayoongozwa na Mkurugenzi mkuu, Nasib Abdul (Dimond Platinum)
Dk. Mwinyi alipokea Salamu hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na kiongozi huyo na ujumbe aliofuatana nao.
Rais Dk. Mwinyi aliushukuru uongozi wa Wasafi uliofika kwa lengo la kumfariji kufuatia msiba wa Baba yake mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassani Mwinyi aliyefariki Februari 29, 2024, Dar es Salaam
na kuzikwa Kijiji cha Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja, Machi, 02 mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine pia, Rais Dk. Mwinyi pia aliwashukuru Wasafi kwa kujitoa kwako na kuungamkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyatangaza mazuri yote yanayofanywa na serikali kupitia Sanaa yao ya muziki.
Naye, Dimond Platinum amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada zake za kuendelea kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa Zanzibar na kusifia jitihada zake wamekua wakizishuhudia kila uchao kupitia mafanikio makubwa kwenye huduma za
jamii ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Alisema hatua za maendeleo zilizofikiwa na Serikali ya Rais Dk. Mwinyi zimevuka malengo ya Ilani ya CCM na Kwenda mbali zaidi. Dimond Platinum ni nyota maarufu wa Sanaa ya muziki wa “bongo Flavor” Tanzania pia ni mwanamuziki aliefanikiwa kuliteka soko la muziki wa kisasa Afika Mashariki, Afrika na dunia kwa ujumla.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.