NI BANDIKA BANDUA LEO NI JIMBO LA SEGEREA MWENEZI MAKALLA AANZA NA UKAGUZI WA JENGO LA SHULE YA GHOROFA MINAZI MIREFU
Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla amekagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kisasa na ya Ghorofa ya Minazi Mirefu iliyopo Jimbo la Segerea na Wilaya ya Ilala .Jengo jipya linalojengwa Lina Madarasa 20 ambayo yako hatua za Umaliziaji .
CPA Makalla amesema Mkoa wa Dar es salam unajengwa Majengo ya Kisasa ya Ghorofa Majengo ya Ghorofa likiwemo Hili la Minazi Mirefu tuna kila Sababu ya kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza kwenye suala la Elimu na sio Jengo hili tu pale Liwiti Jengo la Ghorofa na Wanafunzi wameshaanza kutumia.
🗓08 Julai 2024
Siku ya Tatu Ziara ya Mlezi Mkoa wa Dar es salam