Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
CCM IMEAMUA KUTOA ELIMU KUHUSU MASUALA YALIYOPO MAHAKAMANI - MAKALLA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Amos Makalla amesema kuwa viongozi wengi wa chama wamekuwa wakikutana na jumbe mbalimbali kupitia simu na hata malalamiko kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara kutoka kwa wananchi kuhusiana na kesi ambazo tayari zilishatolewa maamuzi na mahakama.
Kutokana na hayo, Makalla ameeleza kuwa CCM inaamini katika utawala bora wa kuzingatia vyombo vya sheria na kuwa haki ya kutoa haki inapatikana kupitia Mahakama na hakuna mwenye mamlaka ya kuingilia mahakama na ndio maana wakaamua kutoa elimu kwa watu kuwa mahakama ndio chombo pekee cha kutoa haki na hakuna mwenye uwezo wa kuingilia katika maamuzi ndio maana kama hujaridhishwa na maamuzi basi utakata tena rufaa.
Mwenezi Makalla amewataka watanzania kuamini vyombo vya sheria kwa kuwa ndio kazi yake na vinaifanya pasipo kudidimiza.
Makalla ameyasema hayo leo akiwa kwenye kipindi cha #Goodmorning kinachoruka kupitia redio ya wasafi, alipotembelea katika studio za Wasafi Media ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapa Nchini.
🗓️8 Mei, 2024
📍Dar es salaam
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.