KINANA ASHIRIKI IBADA MAALUM YA KUMBUKIZI YA MIAKA 40 YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Bara) Ndg. Abdulrahman Kinana, ashiriki Ibada Maalum ya Kumbukizi ya miaka 40 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine. Ibada hiyo ya Misa Takatifu imefanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine Monduli Mkoani Arusha tarehe 12 Aprili, 2024.