Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza azma yake ya kutaka kusambaza umeme vijiji vyote vya Unguja na Pemba na kukuza maendeleo maeneo hayo.

alternative

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes aliyekuja kujitambulisha.

Kwenye mazungumzo yao, wamegusia maeneo makuu manne ya ushirikiano uliopo baina pande mbili hizo za diplomasia ikiwemo Sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi, Afya na Mazingira.

Kuhusu umeme Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi, Tinnes kuangalia uwezekano wa kuongeza Ushirikiano uliopo baina ya Norway na Tanzania ikiwemo Zanzibar hasa kusambaza umeme vijijini ili kuviendeleza vijiji hivyo.

Akizungumzia sekta ya Mafuta na Gesi, Rais Dk. Mwinyi ameikaribisha Norway kuangalia fursa za uwekezaji kwenye maeneo hayo.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Tinnes kuongeza ushirikiano kwenye sekta ya Afya kupitia hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo.

Akigusia suala za Mazingira Rais Dk. Mwinyi alieleza Zanzibar na Norway zimekua na ushirikinao mzuri kwenye maeneo hayo, sambamba na kuwawezesha na kuwaendeleza wanawake wa Zanzibar.

Dk. Mwinyi pia alimueleza Balozi huyo, kuangalia uwezakano wa kuwaendeleza wakulima wa mwani wa Zanzibar kupitia sekta ya Uchumi wa Buluu.

Alisema, Uchumi wa Buluu ni Sera kuu ya Zanzibar ya kukuza Uchumi wake ikifuatiwa na Utalii unaochangia asilimia 30 ya pato la taifa.

Naye, Balozi Tinnes alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi ushirikiano mzuri uliopo baina ya Ubalozi huo na Shirika la Umeme, Zanzibar (ZECO) kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati ya kukuza huduma za umeme kwa visiwa vya Zanzibar.

Balozi Tinnes alisema, ZECO na Ubalozi wa Norway nchini umefikia mazungumzo mazuri kwenye kuimarisha ushirikiano wao kupitia miradi mbalimbali ya Shirika hilo.

Kuhusu Sekta ya Afya, Balozi Tinnes alimueleza Rais Dk. Mwinyi ushirikino uliopo baina ya hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali kuu ya Norway kuwa pande mbili hizo zinashirikiana kubadilishana uzoefu na kusaidiana wataalamu kwa maeneo tofauti.

Balozi Tinnes pia alisifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Taasisi za kodi za Tanzania ikiwemo Mamlaka ya Mapato Zanzibar, (ZRA) na taasisi ya kodi ya Norway, alisema Tanzania na Norway zinashirikiano kwa kubadilisha uzoefu na utaalamu wa maeneo hayo.

Pia Balozi huyo, alipongeza hatua kubwa ya Maendeleo iliyofikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kupongeza miaka 60 ya ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Tanzania na Norway uliotengeneza historia muhimu kwa jamii za pande zote mbili za ushirikiano kiuchumi na jamii.

alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi