Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka mikakati na kuwaunga mkono wafanya biashara wadogo wadogo na wajasiriamali ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea ya kujipatia kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla wakati alipokuwa akizungumza na wajasiriamali, wafanya biashara wadogo wadogo na Taasisi za Kiseriakli zilizo chini ya Wizara ya Biashara na viwanda Zanzibar katika Viwanja vya Baraza la wawakili Chukwani nje kidogo wa mji wa Zanzibar.
Amesema kuwa kumekuwepo ushirikiano mkubwa baina ya wafanya biashara wadogo wadogo na taasisi za kiserikali zilizo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar jambo ambalo linaendana na azma ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la kuwarahisishia wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa kuzingatia viwango na hali za kimaisha kwa watumiaji.
Mhe Hemed amesema dhamira ya Serikali kwa wafanya biashara ni kuhakikisha biashara zote zinazozalishwa na wafanya biashara wa ndani zinapata soko la uhakika la kuwawezesha kuuza biashara zao kwa urahisi pamoja na kukua kwa pato la taifa.
Mhe. Hemed amewataka wafanya biashara kuendelea kuzitumia fursa za kibiashara zilizopo nchini kwa kuwawezesha vijana kuweza kupata ajira sambamba na kufanya biashara zenye viwango vya hali ya juu ili waweze kuuza ndani na nje ya nchi.
Amesema Serikali ipo tayari kukaa na wafanyabiashara kutatua changamoto zilizopo ili kurahisisha ufanyaji wa biashara na Serikali iweza kupata kodi jambo ambalo litaipelekea Serikali kufikia malengo iliyojiwekea ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia kodi wanazozitoa.
Kwa upande wake Waziri Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. OMAR SAID SHAABAN amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inawaunga mkono wafanya biashara wote wakiwemo wajasiliamali kwa kuwawezesha kupata soko kwa urahisi za biashara zao wanazozalisha.
Mhe. OMAR amesema kupitia ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya hivi karibuni nchini Korea Serikali kupitia Wizara ya Biashara itafaidiaka na ujenzi wa mradi wa kituo cha Kimataifa cha Biashara kinachotarajiwa kujengwa Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B” unguja.
Nae Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ZASCO Dkt. MASOUD RASHID MOHAMMED amewataka wakulima wa mwani kuhakikisha wanalima mwani wenye viwango na kuhakikisha wanaukausha vizuri ili kuendana na soko la Kimataifa.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Hemed Suleiman Abdulla ametembelea mabanda ya wafanya biashara, wajasiriamali pamoja na Taasisi za kiserikali zilizopo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kwa lengo la kujionea kazi na biashara zinazofanywa na wafanya biashara hao.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.