RAIS DK. HUSSEIN ALI MWINYI AIPONGEZA BENKI YA DUNIA KWA KUENDELEA KUIUNGA MKONO TANZANIA KUPITIA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.
Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo, Ikulu Zanznibar alipozungumza na Rais wa Benki hiyo, Ajay Singh Banga na ujumbe wake, wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa 20 wa Mapitio ya benki hiyo, unaotarajiwa kufanyika, ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar.
Dk. Mwinyi alimueleza mgeni wake huyo juu ya Zanzibar inavyonufaika na fursa nyingi kutoka Benki ya Dunia, kupitia miradi ya kimkakati ya maendeleo ikiwemo miradi ya maji safi na utunzaji wa mazingira, umeme vijijini ambayo inatekelezwa Tanzania Bara.
Pia, Rais Dk. Mwinyi alieleza Zanzibar inavyonufaika na miradi ya huduma za jamii unayoungwa mkono na Benki ya dunia ikiwemo miradi ya uzalishaji umeme, maji safi na salama, miundombinu, uwezeshaji wa Wanawake, afya, elimu na Uchumi wa Buluu ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema, Zanzibar imekua na miradi mingi ya maendeleo inayoungwa mkono na Benki ya Dunia kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya benki hiyo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais Dk. Mwinyi alieleza fursa nyengine ambapo Zanzibar inanufaika kutoka Benki ya dunia ni pamoja na kuwajengea uwezo Wanzania kupitia mikutano ya kimataifa, warsha, makongamano pamoja na misaada ya kiufundi. Mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, Rais Dk. Mwinyi alitembelewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, Nathan Balete anaeziwakilisha nchi nyengine tatu za Afrika mbali na Tanzania zikiwemo Malawi, Zambia na Zimbawe.
Naye, Bw. Ajei Banga, alisifu juhudi za Rais Dk. Mwinyi kwa kuimarisha maendeleo na kuboresha huduma bora za jamii kwa wananchi wake na kueleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na benki hiyo ikiwemo Zanzibar. Pia alisifu uzuri wa kisiwa cha Zanzibar na ukarimu wa watu wake waliojikita kwenye kuendeleza maendeleo. Kwa mara ya kwanza, Zanzibar inakua mwenyeji wa Mkutano mkubwa duniani wa Benki ya Dunia utakaohudhuriwa na wageni mashuhuri akiwemo rais wa Benki hiyo, Ajei Banga,
mkutano huo pia unaotarajiwa kuhudhuriwa kati ya wageni 300 hadi 350 wenye lengo la kufanya mapitio ya miradi inayoungwa mkono na benki hiyo, pamoja na mambo mengine pia utaangalia namna bora ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo na namna ya kuongezwa fedha na ruzuku kwa miradi itakayofanya vizuri zaidi kwa mataifa wanufaika.
Zanzibar pia inanufaika fursa za Benki ya Dunia kupitia sekta ya nishati hususani umeme wa jua, upepo na gesi asilia. Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi amekutana na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Mhe. Fahad Rashid Al Marekhi aliyefika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao waligusia uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Qatar pamoja na fursa mbalimbali zilizopo Zanzibar ikiwemo uwekezaji, biashara, utalii, Uchumi wa Buluu, uvuvi, mafuta na gesi pamoja na huduma za kijamii hususani elimu na afya.
Rais Dk. Mwinyi alisema, licha ya sekta hizo kuwepo kwa kiwango kikubwa nchini lakini zinahitaji kuimarishwa zaidi ili kuwaondoshea wananchi changamoto zinazozikabili sekta hizo, hivyo aliomba ushirikiano zaidi ili kuimarisha sekta za maendeleo nchini pamoja na kulisifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Qatar na Tanzania ikiwemo Zanzibar.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
27-10-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
27-10-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
27-10-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
27-10-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
27-10-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
27-10-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
27-10-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
27-10-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
27-10-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
27-10-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
27-10-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
27-10-2025
TAARIFA KWA UMMA
27-10-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
27-10-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
27-10-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
27-10-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
27-10-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
27-10-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
27-10-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
27-10-2025