Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KWA MAAFISA NA WAPIGANAJI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA ILI KUWEZA KUFANYA KAZI KWA UFANISI MKUBWA NA KUFIKIA MALENGO YA MAPINDUZI MATUKUFU YA MWAKA 1964.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua jingo la ofisi ya Utawala la KMKM Kamandi ya kusini Unguja eneo la UNGUJA UKUU Wilaya ya Kati ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu iliyoimara kwa vikosi vya ulinzi na usalama ikiwemo kikosi cha Maalum cha kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) ikiwa ndio azma ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya kuimarisha vikosi vya Ulinzi ili kuendana na mabadiliko yanayojitokeza ulimwenguni pamoja na kuwajengea uwezo na utayari wa ulinzi kwa raia na mali zao.
Mhe. Hemed amesema dhana ya mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 ni kuwaletea maendeleo wananchi wake bila ya ubaguzi wa aina yoyote pamoja nakuimarisha ulinzi wa nchi pamoja na raia na mali zao pamoja na kuimarisha taasisi mbali mbali za kiserikali ili kuwarahisishia wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Makamu wa pili wa Rais amekitaka kikosi cha KMKM kulitunza jingo hili ili liweze kutumika kama lilivyokusudiwa na serikali pia amesema ni vyema Viongozi kuwajibika na kutenda haki kwa kulinda raia na mali zao na kuhakikisha inapambana na wale wote wanaohujumu uchumi kwa kusafirisha bidhaa kwa njia ya magendo jambo ambalo linaleta madhara kwa serikali pamoja na kurejesha maendeleo nyuma.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amevipongeza vikosi vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini pamoja na kuonesha utayari wao wa kujenga miradi ya kimaendeleo ambayo inaisaidia serikali kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi Maalum vya SMZ Ndugu Issa Mahfoudh Haji amesema Mradi wa Ujenzi wa ofisi ya kikosi cha kuzuia magendo Kamandi ya kusini ni muendelezo wa ujenzi wa majengo ya ofisi, Nyumba na Mahanga kwa wapiganaji ikiwa na leongo la kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili askari na maafisa wa KMKM kwa unguja na Pemba.
Amesema kuwa kukamilika kwa Ofisi hii italeta mapinduizi makubwa pamoja na kuwapunguzia changamoto za ofisi lwa Maafisa na Akari wa kikosi cha KMKM ambapo Mradi ambapo umetumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.1 zimetumika kwa usambazaji wa vifaa ambapo mafundi na vibaruawa mradi huko ni askari na maafisa wa kikosi hicho.
Mapema Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka askari na maafisa wa Kikosi cha kuzuia magendo KMKM kufanya kazi kwa uangalifu wa hali ya juu pamoja na kuhakikisha wanapambana na wale wote ambao wanasafirisha magendo kitendo ambacho hurejesha nyuma maendeleo ya serikali.
Amesema kuwa Kamadi ya kusini inakabiliwa na sehemu kubwa na habari ambayo inabandari zisizokuwa rasmi hivyo ni wajibu wa kila askari na afisa kutimiza wajibu wake katika ulizi na usalama wanchi hii.
Mkuu wa Kikosi Maalum cha kuzuia Magendo Zanzibar KMK M Komodoo Azana Hassan Msingiri amemuhakikishia Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar kuwa jingo hili la Kmandi ya Kusini limejengwa na askari na maafisa wa KMKM kwa lengo la kuisaidia serikali katika kujenga majengo ya kisasa ambayo yatawaondolea wapiganaji changamoto za ofisi.
Msingiri amesema kuwa jingo limekamilika kwa asilimia mia moja lakini bado linakabiliwa na changamoto ya fanicha hivyo ameiomba serikali kuwatatulia changamoto hio ili kuleta ufanisi nzuri wa kazi kwa maafisa na wapiganaji wa kikosi hicho.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.