CHATANDA AKUTANA NA WABUNGE WA MAJIMBO WANAWAKE WA CCM NCHINI
📍Dodoma
🗓️ 13 Mei 2024
Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Leo tarehe 13 Mei, 2024 amekutana na Wabunge wa Majimbo Wanawake katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Huu ni Muendelezo wa Mwenyekiti Chatanda kukutana na makundi mbalimbali ya Viongozi Wanawake kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa Wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu mwakani 2025.
Katika kikao hicho Chatanda aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Bara Ndg. Riziki Kingwande (MNEC) na Katibu wa Wabunge Wanawake ambae pia ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa Mhe. Subira Mgalu (MB)