MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEFANYA ZIARA YA USIKU KUKAGUA MIRADI YA UJENZI WA MASOKO MAGHARIBI B
Mhe. Hemed amesema hatua iliyofikia katika ujenzi wa masoko hayo ni ya kuridhisha ambapo amewataka wakandarasi na washauri elekezi kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilika kwa wakati uliopangwa na ubora wa hali ya juu . Amesema mategemeo ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa masoko hayo yakamilike mwishoni mwa mwaka huu ili wafanyabiashara waweze kuyatumia kwa shughuli za kujipatia kipato cha kila siku.
Aidha amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa miongozo anayoitoa katika miradi hiyo pamoja na upatikanaji wa fedha kwa wakati bila ya ucheleweshaji hatua ambayo inawapa moyo wakandarasi kuwa na kasi ya ujenzi huo. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa lengo la kujenga masoko hayo ni kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara na wananchi ili waweze kufanya biashara zao kwa usalama wa afya zao na kuepuka kufanyabiashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha wanatoa elimu na maelekezo kwa wafanyabiashara juu ya namna bora watakavyoyatumia masoko hayo na kuacha kufanya biashara pembezoni mwa barabara kwani Serikali imetumia gharama kubwa kuyajenga masoko hayo hivyo umakini unahitajika katika kuyatumia na kuyatunza masoko hayo.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe. Massoud Ali Moh'd amesema ziara hiyo ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar inaongeza ari na hamasa ya kufanya kazi kwa ustadi wa hali ya juu ili kufiki malengo ya Serikali kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara.
Ameeleza kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekuwa akishahuri na kutoa miongozo inayochangia kuharakisha umalizikaji wa ujenzi wa mradi wa masoko hayo. Kwa upande wake msanifu majengo na mshauri elekezi kutoka Wakala wa Majengo Zanzibar Mhandisi Shadya Fauz Muhamed amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa tayari wakandarasi wapo hatua za mwishoni za kumalizia ujenzi huo na tayari vizimba vimeshaanza kujengwa.
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
02-01-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
02-01-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
02-01-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
02-01-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
02-01-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
02-01-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
02-01-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
02-01-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
02-01-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
02-01-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
02-01-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
02-01-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
02-01-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
02-01-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
02-01-2026
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
02-01-2026
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
02-01-2026
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
02-01-2026
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
02-01-2026
TAARIFA KWA UMMA
02-01-2026