MAKAMO WA PILI AKIZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
CAPTION
Picha No 01, 02, 03 ni :- Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na Wadau mbali mbali wa Sheria pamoja na Wasaidizi wa Sheria wakati akizindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa Mkoa wa Mjini Magharibi uliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil kikwajuni Jijini Zanzibar.
Picha No 04 Ni :- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe. Mwalimu Haroun Ali Suleiman akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Mjini Magharibi uliofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Picha No 05 Ni:- Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora Ndugu Omar Haji Gora akitoa maelezo mafupi kuhusu Msaada wa Kisheria wa Mama Samia katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo kwa Mkoa wa Mjini Magharibi iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Picha No 06 Ni :- Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa akitoa salamu za Mkoa katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar ambapo ameeleza kuwa Serikali ya Mkoa itahakikisha Kampeni hiyo inawafikia walengwa ili kuwasaidia kujua haki zao mbali mbali.
Picha No 07 :- Baadhi ya Viongozi, Wadau wa Sheria na Wasaidizi wa Sheria wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akihutubia wakati akizindua Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa Mkoa wa Mjini Magharibi uliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Press Release
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema kampeni ya huduma ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia inalenga kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria Nchini.
Ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Mkoa wa Mjini Magharibi katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Ameeleza kuwa kampeni hiyo itaimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wasiojiweza ,wanawake, watoto pamoja na makundi mengine yanayoishi katika mazingira magumu ,kuimarisha amani na utulivu na kuleta utengamano wa Kitaifa.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amewaagiza wanaohusika na utekelezaji wa Kampeni hiyo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kupiga vita na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, udhalilishaji na migogoro ya ardhi vitendo ambavyo vimekua vikijitokeza katika jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza viongozi wa Serikali ya Mkoa wakiwemo Madiwani na Masheha kuwa mabalozi wazuri katika kupiga vita vitendo vya kikatili kwa kusimamia haki na sheria katika kufanya maamuzi.
Aidha Mhe. Hemed amewapongeza wasaidizi wa kisheria Nchini kwa kuendelea kuwasaidia wananchi wasiojiweza ili kupata haki zao kwa mujibu wa sheria.
Aidha amewapongeza wadau mbali mbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Mahkama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake kwa mujibu wa Sheria juhudi ambazo zinaleta taswira njema kwa Wananchi kuwa na imani na wadau hao.
Nae waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Harun Ali Suleiman amesema Kampeni hiyo itasaidia kupunguza dhulma, unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika jamii.
Amesema wananchi wengi wanahitaji msaada wa kisheria ambapo ni wazi kuwa wengi wamenufaika na msaada huo wakiwemo wazee wanaofatilia kiinua Mgongo na Pensheni jamii.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idriss Kitwana Mustafa amesema Serikali ya Mkoa itakuwa karibu na wananchi katika kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa ipasavyo kwa lengo la kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia imezinduliwa leo kwa lengo la kuwafikia wananchi hasa wasio na uwezo ikiwa na kauli mbiu isemeyo "Msaada wa kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo "
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
25-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
25-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
25-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
25-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
25-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
25-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
25-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
25-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
25-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
25-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
25-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
25-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
25-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
25-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
25-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
25-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
25-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
25-05-2026