MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR NDG. HEMED SULEIMAN ABDULLA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA WANANCHI WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI KATIKA ZIARA YAKE YA KUIMARISHA CHAMA KATIKA JIMBO HILO
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kusimamia Misingi ya Chama hicho kwa kujenga umoja, mshikamano, heshima na nidhamu pamoja na kuhakikisha CCM inaendelea kushika Dola kila unapofika Muda wa Uchaguzi. Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Jimbo la Kiembesamaki na Jimbo la Dimani Wilaya ya Dimani Kichama.
Amesema Tanzania inajengwa kwa kusimamia misingi ya umoja, mshikamano iliyoasisiwa na waanzilishi wa TANU Marehemu Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na muanzilishi wa ASP Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ambayo inaendelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Mhe. Hemed amewataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Nchini kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo wa kadi za Elektroniki ili kukiendeleza Chama. Amesema Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo huo ambao utakuwa na taafira zote za msingi za mwanachama .
Aidha Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewakumbusha wanachama kulipa ada za uanachama ili kukiendeleza Chama hicho. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kusimamia hali za watendaji wake katika ngazi zote hasa Mashina ambapo amewapongeza Mabalozi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kukisimamia Chama.
Mhe. Hemed amewataka Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kufanya ziara katika maeneo yao ili kujua shida za Wananchi na kusimamia dhamana na jukumu lao la kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025. Aidha amewataka Viongozi hao kusimamia jukumu lao la msingi waliopewa na Chama Cha Mapinduzi la kuwatumikia na kuzishirikisha Kamati za Siasa katika mipango ya maamuzi ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Skuli Chukwani, Ujenzi wa Barabara pamoja ujenzi wa Miundombinu ya maji hatua ambayo itasaidia kumaliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Siasa, Itikadi na Uenezi Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amemshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa ziara yake hiyo ambayo inaonesha wazi utayari wa Viongozi wakuu wa CCM katika kukiimarisha Chama. Nao Viongozi wa Mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi ya Majimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa wameeleza kuwa ni wajibu wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali zote mbili zinazoongozwa na CCM na kuwataka vijana kuwa mstari wa mbele kueleza mema hayo na kuacha kusikiliza maneno yasio na ukweli.
Katika Ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati ya Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amepokea Taarifa ya utekelezaji wa Jimbo la Kiembesamaki na Jimbo la Dimani, amekagua Ujenzi wa Tawi la CCM Michungwani, ujenzi wa Ofisi za CCM Jimbo la Dimani.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
04-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
04-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
04-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
04-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
04-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
04-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
04-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
04-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
04-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
04-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
04-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
04-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
04-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
04-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
04-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
04-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
04-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
04-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
04-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
04-11-2025