Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
BALOZI DKT. NCHIMBI AHIMIZA UMOJA, AWATAKA WATANZANIA KUTOKUBALI KUGAWANYWA.
"Mafanikio tuliyopata tangu uhuru , tangu Muungano wa Nchi zetu ni kwasababu ya umoja wetu"
"Tusikubali kuacha umoja wetu nawaombeni sana , kama kuna jambo mkienda nyumbani leo na mtu akakuuliza Katibu Mkuu amesema nini umwambie amesema tusikubali kuacha umoja wetu, tusikubali kugawanywa , tusikubali kufarakanishwa"
"...Tanzania lazima iendelee kuwa Nchi moja yenye mshikamano, yenye upendo ambayo haibagui watu wake kwa misingi ya ukabila, wala dini wala vyama vya siasa"
"Wote ni Watanzania, Nchi ni yetu sote tuishi kwa kushirikiana na tupendane...CCM OYEEE! "
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea mikoa 5.
🗓️29 Mei, 2024
📍Manyoni - Singida
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.