Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


HATUWEZI KUJENGA CHAMA CHA WATU WENYE NONGWA - BALOZI DKT. NCHIMBI
 

alternative

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama na viongozi kuwa na nongwa jambo ambalo linapelekea kupoteza upendo, umoja na mshikamano na kutengeneza makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameyasema hayo kwenye mkutano wa ndani uliokutanisha viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia ngazi ya mashina, Viongozi wa Serikali, Taaisi zisizo za kiserikali, Wazee na Viongozi wa dini.

"Umoja kwa wanachama na viongozi na jambo la muhimu na kwa kadri inavyowezekana muhakikishe suala hilo linakuwa la msingi na la kwanza baina yenu"

"Tukienda kwenye chaguzi zetu na tukimaliza chaguzi mambo ya huko yaishe, msijikite katika kuendelea nayo"

"Nongwa za uchaguzi ziishe , unakuta chaguzi zimeisha miaka 4 iliyopita lakini unakuta mtu bado ana nongwa kuanzia aliyeshinda hadi aliyeshindwa, hatuwezi kujenga Chama cha watu wenye nongwa"

Aidha, Amepongeza tabia ya baadhi ya viongozi na wanachama kuwa na msimamo na kutoyumbishwa daima na badala yake kusimamia kwenye kuzingatia katiba na miongozo ya Chama Cha Mapinduzi"

Sambamba na hilo Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu. Damas Ndumbaro ametoa salamu za pongezi kwa niaba ya wananchi wa Songea mjini kwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa kuaminia na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Ndugu. Ndumbaro amesema wananchi wa Songea wakati wote wanaendelea kumuona Balozi Dkt. Nchimbi kama mbunge wao kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuendelea kuwa sehemu ya kuwasaidia.

Aidha, Ndugu. Ndumbaro amesema wananchi wa songea mjini wakati wote hawatayumba na wataendelea kuwa mstari wa mbele katika kusemea kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Rais Samia.

Vilevile, Ndugu. Ndumbaro amewasilisha changamoto ya wananchi wa songea mjini ya kuhitaji kupata barabara unganishi za kiwango cha lami kwa kuunganisha Ruvuma na Mkoa wa Morogoro na Ruvuma na Nchi jirani ya Msumbiji.

🗓️20 Aprili, 2024
📍Songea Mjini - Ruvuma

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi