Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
ZIARA YA NDUGU RABIA ABDULLA HAMID MOHAMMED MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NCHINI CUBA
Ndugu Rabia Mohammed Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa HKT - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa amekuwa na ziara ya siku 4 nchini Cuba ambapo pamoja na mambo mengine amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba (PCC) na Serikali.
Awali Ndg. Rabia alikutana na kufanya mazungumzo na Ndg. Emilio Ratmir Lozada Garcia Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa wa PCC. Ndugu Rabia Mohammed amekutana na kufanya mazungumzo na Komredi Dkt. Roberto Morales Ojeda Mjumbe wa Kamati Kuu (Politiburo), Katibu Mkuu wa Pili na Katibu wa Oganaizesheni wa Chama cha PCC. Wakati uo huo Ndg. Rabia amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Elio E. Rodríguez Perdomo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba.
Viongozi wengine ambao amekutana nao na kufanya nao mazungumzo ni pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuia za Wanawake na Vijana wa Chama cha PCC na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Chama cha Kikomunisti cha Cuba (PCC).
Mazungumzo ya Ndg. Rabia Mohammed yamejikita katika kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha Cuba (PCC), kujenga na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Cuba na kubadilishana uzoefu katika maeneo kadhaa kwa Maslahi ya Nchi na Mataifa yetu mawili.
Katika ziara hiyo Ndg. Rabia ameambatana na Mhe. Humphrey H. Polepole, Balozi na Mkuu wa Kituo cha Uwakilishi Havana na Maafisa Ubalozi.
Imetolewa na,
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🇹🇿 - Havana
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.