Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Wazazi na walezi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa walimu wa madrasa na walimu wa skuli pamoja na kujua taarifa na mienendo ya watoto wao ili kupata wataalamu na wanazuoni wabobezi wa baabae.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid IITISWAM uliopo TUNGUU KWA SHEMEGO Wilaya ya Kati Unguja mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema kuwa kuwafatilia vijana katika suala zima la kupata elimu zote mbili kutapelekea kupata walaalamu watakao weza kulisaidia Taifa katika kusimamia miradi mbali mbali ya kimaendeleo pamoja na kupata wanazuoni watakao watakaoitetea dini ya kiislamu kwa ushahidi wa Qur-an na Sunna.
Alhajj Hemed amesema suala la wazazi na walezi kuwasiamamia vijana katika mambo mema yakiwemo suala la Elimu na Ibada ni suala la lazima kwani kufanya hivyo ni kutimiza wajibu wao na kujiweka huru na masuala mbele ya M.Mungu kwani kila mzazi ni mchunga juu ya mtoto wake.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa maisha ya duniani ni mapito tu hivyo ni lazima kujiandaa kwa kufanya Ibada pamoja na kuwaandaa watoto katika suala zima la kuwapatia elimu yenye manufaa hapa duniani na kesho akhera.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewataka wazazi na walezi kuwafuatilia watoto wao wanaoingia skuli katika mkondo wa jioni kwa skuli ambazo bado wanafanya hivyo kwani serikali ya awamu ya Nane (8) inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Mwinyi inahakikisha inaendelea kujenga skuli za ghorofa kila sehemu ili kuwawezesha wanafunzi kusoma mkondo mmoja tu na kupata elimu iliyobora kwa maslahi ya taifa.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Ustadh. RAJAB R’DHAN CHOUM amewaasa waumini wa Dini ya Kiislam hasa wale waliomo kwenye Ndoa kuacha tabia ya kutoa Talaka kiholela jambo ambalo linamkirihisha sana Allah (S.W) na kupelekea kuwasambaratisha watoto na kukosa malezi yaliyo bora kutoka kwa wazazi wawili.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi kususiana watoto wanapoachana huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki zao za msingi na kupelekea Taifa kuwa na watoto wengi wa mtaani na kuongezeka kwa mambo maovu na machafu baina yao.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.