Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Wananchi wametakiwa kudumisha umoja na mashirikiano baina yao na kusaidiana kwa kila hali kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya chake chake Mhe. Abdalla Rashid Ali kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba katika ftari iliyoandaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla kwa ajili wa wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba .
Amesema mkusanyiko huo uliojumuisha wananchi wa maeneo mbali mbali unadhihirisha kuwepo kwa umoja,mshirikiano na upendo baina yao jambo ambalo linapelekea serikali kupiga hatua na kufikia maendeleo endelevu.
Mhe. Abdalla amesema Wazanzibar wanatakiwa kuienzi rasilimali ya amani na utulivu iliyopo nchini kwani ndio tunu ya Watanzania ambayo baadhi ya nchi wameikosa hivyo ni lazima kuitunza na kuienzi ili kuwarahisishia viongozi wakuu kuyatekeleza kwa vitendo yale yote walioyaahidi kwa wananchi wake.
Aidha amewasisistiza wananchi kuenzi kwa vitendo falsafa na fikra za viongozi wa kuu wanchi katika kushirikiana baina yao ili kupiga hatu za kimaendeleo na kuondosha changamoto zilizopo.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa amewataka wafanya biashara kuendelea kufanya biashara zao kwa kufata bei elekezi zilizowekwa na Serikali hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kipindi ambacho imezoeleka bidhaa nyingi za muhimu kupanda bei na kusababisha baadhi wa wananchi kutomudu kununua mahitaji yao ya ftari.
Aidha amesisitiza kuwa Serikali za Mkoa na Wilaya hazitosita kumchukulia hatua za kisheria mfanya biashara yoyote ambae atakwenda kinyume na maelekezo ya Serikali ya kufata bei elekezi katika biashara yake kwani kufanya hivyo ni kuizarau serikali pamoja na kuwaumiza wananchi.
Akitoa neno la shukrani ndugu SHARIF MAKAME TAI kutoka Wilaya ya Wete kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba amemshukuru Makamu wa pili wa Rais kwa kuendeleza kawaida yake ya kuwafutarisha wananchi wa mikoa miwili ya Pemba kwani kufanya hivyo ni kufuata Sunna za Mtume Muhamad (S.A.W).
Imekuwa ni kawaidi kwa kila mwaka ifikapo Mwezi mtukufu wa ramadhani, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla kujumuika na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba kuftari nao pamoja .
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.