KULIIBIA TAIFA NI KUJIIBIA MWENYEWE - BALOZI DKT. NCHIMBI
> Akemea tabia ya wizi na vitendo vya RUSHWA
> Awataka TAKUKURU kuendelea kufuatilia matumizi ya fedha ya miradi yote nchini
> Asisitiza matumizi sahihi ya fedha katika miradi ya serikali
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekemea tabia ya wizi na kulaani vikali watu wote wenye tabia ya wizi na vitendo vya rushwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani ya makambako mkoani Njombe, Balozi Dkt. Nchimbi amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa na kukemea tabia ya vijana kutofanya kazi na badala yake kujikita kwenye tabia za kufanya kazi zisizo halali.
Akitoa majibu ya kero za wananchi kuhusiana na tabia ya wizi na ujangili, Balozi Dkt. Nchimbi amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ndug. Mtaka kufanya uchunguzi ili kubaini vinara wa ujambazi na mauji kwa lengo la kuthibiti kabisa tabia hizo.
Vilevile, Balozi Dkt. Nchimbi amewataka viongozi wote wa serikali kuwa na matumizi sahihi ya fedha za umma na kuwataka TAKUKURU kuendelea na kazi yao nzuri ya kufuatilia miradi yote ya kimaendeleo kuanzia inavyoanza hadi kukamilika kwake.
" Mkoa wa Njombe mmepata Tsh Bilioni 900 hela hizo ni nyingi sana na nitumie nafasi hii kuwapongeza Mkuu wa mkoa na wabunge wenu kwa kutengeneza ushawishi wa kumfanya Rais Dkt. Samia kutoa fdha hizo ndani ya mkoa wenu "
" Vyombo vyote vya serikali vyenye mamlaka ya matumizi ya fedha za miradi hakikisheni pesa hizo zinatumika kihalali na msisubiri kukamata walioiba bali ni lazima mdhibiti na kuzuia mianya ya uibaji "
" TAKUKURU hakikisheni miradi yote hasa mikubwa ya maendeleo mnaifuatilia tangu ikiwa inaanza kuhakikisha hakuna fedha ya umma inaibiwa na kutumika vibaya, tunataka thamani ya fedha ieandane na thamani ya mradi husika "
ποΈ18 Aprili, 2024
πMkutano wa Hadhara Makambako - Njombe
π°VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
25-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
25-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE β KIBAHA
25-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
25-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
25-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
25-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
25-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
25-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
25-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
25-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
25-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
25-05-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
25-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
25-05-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
25-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
25-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
25-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
25-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
25-05-2026