Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
PINDI CHANA AMUHAKIKISHIA BALOZI DKT. NCHIMBI KUWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA INAWAFAKIA WATANZANIA WOTE, NAYE RC MTAKA AMUELEZA KUWA VIONGOZI THABITI WA NJOMBE NI FAIDA YA UWEKEZAJI WA CCM
Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Pindi Chana, amemuhakikishia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ya kwamba kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) inawafikia watanzania wote kila kona ya nchi na kuwasaidia katika mambo yote yanayohitaji msaada wa kisheria na kumwambia kuwa kampeni hiyo imesaidia kungeza uelewa kwa watanzania wengi na kuona umuhimu wa kuzingatia na kufuata sheria na taratibu za nchi.
Akizungumza mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya stendi za zamani ya Makambako mkoani Njombe katika muendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu, Balozi Pindi Chana ameitambulisha kwa Katibu Mkuu na Wananchi wote timu ya kikosi kazi maalum inayozunguka katika kutoa msaada huo wa kisheria kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
" Hatulali tupo mtaa kwa mtaa, tunafika nyumba kwa nyumba mpaka kieleweke kuhakikisha watanzania wanapatiwa msaada wa kisheria na ndio kazi tuliyotumwa na Rais wetu kwa mapenzi yake ya dhati kwa Watanzania wote " Alisema Balozi Dkt. Pindi Chana.
Naye RC Mtaka amueleza Balozi Dkt. Nchimbi kuwa viongozi thabiti wa Njombe ni faida ya uwekezaji wa CCM.
> Asema Bilioni 900 zimetumika kwa maendeleo mkoani Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ndugu. Anthony Mtaka , amemueleza Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Viongozi thabiti na imara wa mkoa wa Njombe ni faida iliyotokana na zao la uwekezaji wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia Chipukizi hadi Vijana.
RC Mtaka ameyasema hayo mbele ya Maelefu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa stendi ya zamani ya makambako kwa ajili ya ushiriki wao kwenye mkutano wa hadhara.
Pia, RC Mtaka amemueleza Balozi Dkt. Nchimbi kuwa Maendeleo yaliyopo mkoani Njombe katika kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Rais Dkt. Samia ambapo amesema kiasi cha Tsh Bilioni 900 kimetumika kwa maendeleo katika sekta mbalimbali.
"Njombe kuna matunda ya watu uliowalea ukiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na haya yote ni mafanikio ya uwekezaji wa CCM kwa Chipukizi na Vijana"
"Tunakuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kulinda heshima ya CCM ndio maana madiwani, wabunge, wenyeviti wa serikali za mitaa na viongozi wa chama wote wana ushirikiano wa timu moja katika kazi"
"Njombe kazi kubwa imefanyika na katika kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeletwa fedha Tsh Bilioni 900 na kutumika katika sekta zote za mendeleo ya kijamii (afya, maji, umeme (85% zaidi vijiji vyote vina umeme),)
"Makambako ni eneo la uwekezaji wa kibiashara na litapelekea kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa wananchi wa Njombe"
🗓️18 Aprili, 2024
📍 Makambako - Njombe
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.