Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
ILALA IMECHACHAMAAA, MWENEZI MAKALLA AANZA NA UKAGUZI WA JENGO LA SHULE YA GHOROFA MNAZI MMOJA NA UKAGUZI WA BARABARA 20 ZA MITAA ILALA
Katibu wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla amekagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kisasa na ya Ghorofa ya Mnazi Mmoja iliyopo Jimbo la Ilala Jengo jipya linalojengwa Lina Madarasa 20 yenye thamani ya Bilioni 1.8 pamoja na Ukaguzi wa Barabara 20 za Mitaa ya Ilala zilizo gharimu Bilioni 30 kandarasi zote zipo hatua ya Umaliziaji
CPA Makalla amesema Mkoa wa Dar es salam unajengwa Majengo ya Kisasa ya Ghorofa likiwemo la shule ya Mnazi mmoja, nyingi za Mkoa wa Dar es salam huku barabara zinaendelea kujengwa hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mikakati ya kuibadilisha Dar es salam na kulifanya Jiji la Kisasa.
🗓09 Julai 2024
Siku ya Nne Ziara ya Mlezi Mkoa wa Dar es salam
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.