MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA AMEWATAKA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUSIMAMIA MISINGI YA CHAMA HICHO KWA KUJENGA UMOJA, MSHIKAMANO, HESHIMA NA NIDHAMU PAMOJA NA KUHAKIKISHA CCM INAENDELEA KUSHIKA DOLA KILA UNAPOFIKA MUDA WA UCHAGUZI.
Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Jimbo la Kiembesamaki na Jimbo la Dimani Wilaya ya Dimani Kichama.
Amesema Tanzania inajengwa kwa kusimamia misingi ya umoja, mshikamano iliyoasisiwa na waanzilishi wa TANU Marehemu Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na muanzilishi wa ASP Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ambayo inaendelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Mhe. Hemed amewataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Nchini kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo wa kadi za Elektroniki ili kukiendeleza Chama.
Amesema Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo huo ambao utakuwa na taafira zote za msingi za mwanachama.
Aidha Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewakumbusha wanachama kulipa ada za uanachama ili kukiendeleza Chama hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kusimamia hali za watendaji wake katika ngazi zote hasa Mashina ambapo amewapongeza Mabalozi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kukisimamia Chama.
Mhe. Hemed amewataka Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kufanya ziara katika maeneo yao ili kujua shida za Wananchi na kusimamia dhamana na jukumu lao la kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.
Aidha amewataka Viongozi hao kusimamia jukumu lao la msingi waliopewa na Chama Cha Mapinduzi la kuwatumikia na kuzishirikisha Kamati za Siasa katika mipango ya maamuzi ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa Miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Skuli Chukwani, Ujenzi wa Barabara pamoja ujenzi wa Miundombinu ya maji hatua ambayo itasaidia kumaliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Siasa, Itikadi na Uenezi Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amemshukuru Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa ziara yake hiyo ambayo inaonesha wazi utayari wa Viongozi wakuu wa CCM katika kukiimarisha Chama.
Nao Viongozi wa Mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi Ngazi ya Majimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa wameeleza kuwa ni wajibu wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali zote mbili zinazoongozwa na CCM na kuwataka vijana kuwa mstari wa mbele kueleza mema hayo na kuacha kusikiliza maneno yasio na ukweli.
Katika Ziara hiyo Mjumbe huyo wa Kamati ya Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amepokea Taarifa ya utekelezaji wa Jimbo la Kiembesamaki na Jimbo la Dimani, amekagua Ujenzi wa Tawi la CCM Michungwani, ujenzi wa Ofisi za CCM Jimbo la Dimani.
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐓𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐘𝐀𝐌𝐀 𝐓𝐀𝐖𝐀𝐋𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀
22-07-2026
𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
22-07-2026
🚆 𝐓𝐔𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀!
22-07-2026
ZIARA YA RAIS WA MISRI-TANZANIA
22-07-2026
🔰 CCM NA ACT-WAZALENDO WASAINI MARIDHIANO YA PAMOJA YA KISIASA ZANZIBAR
22-07-2026
🎉 𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐊𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐖𝐀, 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐒𝐇𝐀-𝐑𝐎𝐒𝐄 𝐌𝐈𝐆𝐈𝐑𝐎! 🔰
22-07-2026
🔰𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐁𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐇𝐀𝐋𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀
22-07-2026
🔰𝐇𝐄𝐑𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐇𝐈𝐌𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝟐𝟎𝟐𝟔!
22-07-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐏𝐖𝐀𝐍𝐈; 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!!!!!
22-07-2026
𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐌𝐏𝐀 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀
22-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐋𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐄𝐑𝐄𝐊𝐄𝐓𝐖𝐀 𝐌𝐋𝐀𝐍𝐃𝐄𝐆𝐄, 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐒𝐀-𝐈𝐑𝐈𝐍𝐆𝐀
22-07-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟏𝟎 𝐌𝐀𝐅𝐈𝐅𝐈, 𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈𝐓𝐈𝐙𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈, 𝐔𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐍𝐀 𝐌𝐒𝐇𝐈𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
22-07-2026
𝐌𝐑𝐀𝐃𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐘𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎 𝐊𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀 𝐅𝐔𝐑𝐒𝐀 𝐙𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐉𝐀𝐍𝐀
22-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎, 𝐙𝐀𝐌𝐔 𝐘𝐄𝐍𝐔 𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎!
22-07-2026
𝐑𝐀𝐁𝐈𝐀: 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐒𝐔𝐋𝐔𝐇𝐔 𝐇𝐀𝐒𝐒𝐀𝐍 𝐍𝐈 𝐌𝐓𝐄𝐊𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐇𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐀𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌
22-07-2026
𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐈𝐌𝐄𝐈𝐓𝐀, 𝐍𝐄𝐄𝐌𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐙𝐈 𝐊𝐈𝐋𝐎𝐋𝐎!
22-07-2026
𝐑𝐔𝐀𝐇𝐀 𝐌𝐁𝐔𝐘𝐔𝐍𝐈 𝐘𝐀𝐅𝐔𝐑𝐈𝐊𝐀; “𝐂𝐇𝐈𝐄𝐅 𝐂𝐇𝐎𝐆𝐀𝐕𝐀𝐓𝐀𝐌𝐁𝐔𝐋𝐄” 𝐀𝐊𝐈𝐓𝐄𝐊𝐀 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀!
22-07-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐔𝐌𝐖𝐀𝐆𝐈𝐋𝐈𝐀𝐉𝐈 𝐍𝐈 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐔𝐂𝐇𝐔𝐌𝐈 𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
22-07-2026
𝐂𝐂𝐌 𝐘𝐀𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐌𝐊𝐎𝐍𝐎 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐉𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐙𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀𝐉𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈
22-07-2026
𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐍𝐈 𝐌𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎: 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈
22-07-2026