Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. HEMED SULEIMAN ABDALLAH AFANYA ZIARA YA KICHAMA JIMBO LA MFENESINI.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewataka Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha vijana waliotimiza umri wa miaka 18 wanajiandikisha ili kupata kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kukichagua na kukipa ushindi chama hicho ifikapo uchaguzi mkuu wa nchi mwaka 2025.
Mhe. Hemed ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi katika ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Jimbo la Mfenesini,Jimbo la Mwera pamoja na Jimbo la Welezo Wilaya ya Mfenesini Kichama.
Amesema Viongozi wa ngazi mbali mbali katika majimbo hayo ndio kiunganishi kizuri ambacho kitaweza kukivusha chama Cha Mapinduzi ifikapo uchaguzi mkuu wa nchi hivyo ni lazima kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo wanachama wa chama hicho pamoja na kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya wenye kukiletea ushindi chama cha mapinduzi.
Amesema Viongozi wanajukumu la kuimarisha umoja na Ushirikiano baina Yao kama iliyoasisiwa na waanzilishi wa TANU na ASP Marehemu Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ambapo misingi hio inaendelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa sasa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Katika kukiimarisha chama hicho Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ameweka jiwe la msingi la tawi la chama hicho Makufuli jimbo la welezo , tawi la CCM Mtopepo na kushiriki ujenzi wa Soko dogo Chuwini na ujenzi wa Tawi la CCM jimbo la Mwera Mwembe Mchomeke.
Aidha Mhe. Hemed amewataka Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Viongozi wakuu wa chama Cha Mapinduzi katika kuitekeleza vyema ilani kwa kuwaletea Maendeleo Wananchi wake ikiwemo ujenzi wa miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Tanzania inapiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na dhamira njema ya Viongozi wake wenye chachu ya mabadiliko kwa wananchi wao.
Akizungumza usajili wa kadi za chama kwa njia ya eletroniki Mjumbe huyo wa kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Amesema Dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha wanachama wote wanasajiliwa katika Mfumo huo ambao utakuwa na taafira zote za msingi za mwanachama .
Aidha Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amewakumbusha wanachama kulipa ada za uanachama ili kukiendeleza Chama hicho.
Sambamba na hayo mjumbe huyo wa kamti kuu ya halmashauri kuu ya ccm taifa ameeleza kuwa chama cha mapinduzi na Uwongizi hakitamfumbia macho mtu yoyote ambae atakwenda kinyume na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa lengo la kukichafua Chama kwa maslahi yake binafsi ama watu wachache wasikipendelea mema chama hicho.
Aidha amekemea vikali wale wote walionza chokochoko za kupanga safu za uongozi hasa wabunge na wawakilishi na kusema kuwa muda wa kufanya hivyo haujafika na badala yake watumie muda wao kuzidi kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya Shina hadi Taifa.
Aidha amewataka Viongozi wa majimbo kusimamia jukumu lao la msingi waliopewa na Chama Cha Mapinduzi la kuwatumikia na kuzishirikisha Kamati za Siasa katika mipango ya maamuzi ili kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi wao.
Katika Ziara hiyo ya kukijenga chama mjumbe huyo wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM taifa Ndugu Hemed ameshiriki ujenzi wa soko dogo LA chuwini linalojengwa kwa mfuko wa jimbo pamoja na ujenzi wa tawi la CCM Mwembe Mchomeke
Nae Katibu wa Itikadi na uwenezi Ndugu.Khamis Mbeto amewataka wanachama wa CCM kuachana na tofauti zao na kuacha makundi yasio na tija katika chama na kuelekeza nguvu zao zote katika kuwatumikia na kutekeleza ahadi zao kama ilani ya Chama Cha Mapinduzi Inavyoelekeza.
Amesema mgawanyiko katika chama ni jambo la kukemewa kwani hautakiimarisha chama bali utazorotesha mipango ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla .
Nao viongozi wa majimbo wamempongeza mwenyetiki wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuisimamia vyema ilani ya chama hicho kivitendo.
Hata hivyo viongozi hao wameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaletea maendeleo wananchi yake pamoja na kuwajengea miradi mbali mbali ya kimkakati katika majimbo yao..
Ziara hiyo ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ametembelea jimbo ya Mfenesini, jimbo la Mwera na Jimbo la Welezo pamoja na kuweka mawe ya msingi kwenye Matawi ya chama hicho, ikiwa na lengo la kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.