CCM YAMCHANGIA LISSU SHILLINGI MILLIONI TANO -UNUNUZI WA GARI
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. John Nchimbi,akishuhudia Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) - Oganaizesheni,Issa Ussi Haji Gavu akionesha zaidi ya Sh. Mil. 5 zilizochangwa na Wana CCM Pamoja na Wananchi katika Mkutano wa hadhara wa CCM, za kusaidia matengenezo ya gari bovu la Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Antipas Tundulisu. Tukio hilo limetokea leo Alhamis Agosti 15, 2024 kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza,wakati Balozi Nchimbi akihitimisha leo ziara yake ya siku mbili jijini humo.Kulia ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla.