Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kupata kizazi chenye hofu ya Allah kitakachosaidia kuziondosha changamoto zilizopo zinazosababishwa na kukosekana kwa maadili mema kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid JAMII WATHABATUL- KHEIR iliyopo KOANI kwa KOZI Wilaya ya Kati mara baada ya kumaliza Ibada ya Sala ya Ijumaa.
Amesema ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuwalea watoto wao katika maadili mema yatakayowajenga kidini na kiimani jambo ambalo litasaidia Taifa kupata viongozi bora wa baadae na wenye kufanya kazi zao kwa hofu ya Mwenyezi Mungu.
Alhajj Hemed amesema wakati umefika wa jamii kujitathmini katika malezi wanayowalea watoto wao ili kupunguza malalamiko ya mmong’onyoko wa maadili unaopelekea vijana kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Sambamba na hayo Alhajj Hemed ameendelea kuwasisitiza wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla kuzidi kudumisha Amani na Utulivu uliopo nchini jambo ambalo huwaweka huru katika kufanya shuhuli zao mbali mbali za kujitafutia maisha kwa faida yao na Taifa kwa ujumla.
Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Sheikh SALIM MASSOUD SEIF amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kuendelea kuzilea vyema familia zao ili kuweza kupata watoto wema ambao watakuwa wema sasa na hadi kuondoka kwao duniani.
Amesema kuwa waislamu ni lazima kushirikiana na kuamrishana mambo mema na kukatazana mabaya ili kujikurubisha karibu na Allah (S.W) na kufikia lengo la kuumbwa mwandamu hapa duniani
Niwapongeze Umoja wa Wanawake Tanzania kwa mambo matatu makubwa; UWT imefanya kazi kubwa ya kutayarisha viongozi, kubadilisha mitazamo ya wanawake wa Tanzania na kusimama kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni ukweli usiopingika kwamba mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa na mustakabali wa Taifa, ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi.