Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


KINANA AWATAKA VIONGOZI WA CCM MARA KUTOKUBEBA AU KUPANDIKIZA WAGOMBEA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 NA UCHAGUZI MKUU 2024.

alternative

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara ndugu Abdullahman Kinana amewataka viongozi wa Chama hicho Mkoa wa Mara kutokubeba wagombea au kupandikiza wagombea kwa njia yoyote ile kuelekea Chaguzi mbili za Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mapema August 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025 

Kinana ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri iliyoboreshwa Wilaya ya Serengeti April 14, 2024 akiwa katika ziara ya kikazi hasa kwa kuzingatia yeye ni Mlezi wa Mkoa wa Mara.

Mwaka huu wa 2024 maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025 tayari yameanza na hivyo Kinana amewakumbusha wana CCM kote nchini wakiwemo wa Mkoa wa Mara kutenda haki katika chaguzi huku akisisitiza kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtu.

Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya Viongozi ambao wamekuwa wakitoa rushwa kupata uongozi ikiwemo viongozi wanaopekea rushwa ambapo amesistiza vitendo vya rushwa vinasababisha kupata viongozi wanaoshindwa kuitumikia jamii

alternative alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi