Makao Makuu - Dodoma
#CCM Imetimia KaziIendelee

Habari na Matukio Mbalimbali


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi Kuifungua kiuchumi Pemba

alternative

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr.Hussein Ali Mwinyi amesema serikali ina mpango wa kuifungua kiuchumi kisiwa cha pemba kupitia maeneo manne ya ujenzi ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kisiwa hicho

Kauli hiyo ameitoa juzi tarehe 17 July wakati akizungumza na mabalozi, wajumbe wa halmashauri kuu za majimbo,wilaya na mkoa wa kusini Pemba katika ukumbi wa Umoja ni nguvu uliopo mkoani. Raisi Dk.Mwinyi aliyataka maeneo mengine ambayo yataichochea kuifungua Pemba kiuchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, bandari na maeneo huru ya uwekezaji. Katika maelezo yake Raisi Dk.Mwinyi ambae ni Makamu Mwenyekiti wa ccm Zanzibar alisema serikali ina azma ya kuifungua Pemba kiuchumi kwa miradi maalum, '' Ukitaka kuifungua nchi ni miundombinu na hapa Pemba tunajenga kiwanja cha ndege chenye urefu wa kilomita 2.5, sinashaka ndege kubwa zitakuwa zinakuja hapa moja kwa moja kutoka nje, hivyo kitakuwa kiwanja cha kimataifa'' alisema.

Alisema serikali ikimaliza ujenzi wa kiwanja cha ndege kisiwani Pemba pia itajenga jengo jipya na kubwa la abiria katika kiwanja hicho, Rais Dk.Mwinyi alisema kwa upande wa miundombinu ya barabara kuu serikali inaendelea na mpango wake wa ujenzi wa barabara ya chakechake, wete na mkoani na barabara za ndani '' Barabara zote hizo zipo katika mpongo wa utekelezaji na sina ya shaka kuwa barabara hizi zitakuwa nyingi na bora zaid'' Alisema. Alisema eneo jengine ni ujenzi wa bandari ambapo serikali inatarajia kuanza na bandari ya mkoani na kufuatia na bandari ya wete ''lakini sasa hivi upembuzi yakinifu unafanyika bandari ya wete na ujenzi wa bandari hizi itasaidia kushuka kwa gharama za bidhaa kisiwani hapa kutokana na kuwa bidhaa hazitoki moja kwa moja , hivyo hivi sasa bidhaa zitatoka moja wa moja kutoka nje ya nje'' Alisema, Alisema gharama za bidhaa zinapanda kutokana na gharama za usafirishaji wa bidhaa hizo ambazo mara nyingi hutoka Unguja, Mombasa na Dar-es-salam ndipo zifikie kisiwani Pemba. 

Rais Dk.Mwinyi alisema baada ya bandari hizo kujengwa itawezesha meli kubwa kutoka nje ya nchi kuja kuleta bidhaa hizo kisiwani Pemba, alisema eneo la mwisho la kuifungua Pemba kiuchumi ni kutengeneza maeneo huru ya uwekezaji ambapo tayari serikali imekwisha anzisha eneo hilo micheweni ''Hivi karibuni serikali itatengeneza barabara yenye kiwango cha lami katika eneo hilo ili sasa tuwe tayari kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza viwanda kisiwani Pemba'' alisema. Alisema baada ya hatua hiyo pemba itabadilika na kuwa eneo la utalii na viwanda 

Kwa upande wa naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Mohammed Said Mohammed (Dimwa) alisema utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ndio inayowavuta wapizani kujiunga na chama ''Kinachowautia pia ni utendaji wako muheshimiwa makamo mwenye kiti uliyotukuka ambao kwa kiasi kikubwa umeleta maendeleo kwa wazanzibari'' alisema. Alisema mbali na wapinzani hao wawili waliojitokeza kujiunga na ccm bado kuna kundi kubwa la wapinzani wanataka kujiunga na chama kutokana na maendeleo aliyoyafanya Dk.Mwinyi kwa kipindi kifupi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya uwana chama na raisi Nasour Seif mwanachama wa ICT Wazalendo ambae alikuwa miongoni mwa wanzilishi wa chama cha CUF alisema ameamua kujiunga na CCM kutokana na maendeleo yanayofanywa, pia alisema mpka sasa zanzibar imekuwa na miundombinu mengi yenye kuleta tija katika ukuwaji wa kiuchumi '' Ukiangalia bajeti ya zanzibar imeongezeka  kutoka Sh.trilioni moja hadi kufikia trilioni mbili ikiwa ni ongezeko la asilimia 16 ambaapo zaid ya asilimia 83 ya bajeti hiyo ni kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar'' alisema. Alisema hakuna chama cha siasa cha kweli chenye kuleta maendeleo kwa wanachi kama ccm na kwamba vyama vyengine vipo kimaslahi. ''Naomba wamaccm mtupokee na mtupe mashirikiano kwa ajili kukiendeleza chama chetu'' alisema.

alternative alternative alternative
Habari Nyingine

Nukuu za Viongozi